Nikumbushe(Cover) Lyrics

GLORY SHAVU Tanzanie | Gospel,

Nikumbushe(Cover) Lyrics


Ninahisi kinywa kujawa na lawama tele
Pale mambo yanapoonekana hayaendi 
Ni ajabu sana namna moyo unahangaika(Natafuta majibu)
Ajabu sana moyo unapoonyesha mashaka

Ya kwamba japo kuwa Mungu
Anaishi ndani yangu, kuna muda nahofu
Ya kwamba japo kuwa Mungu
Anaishi ndani yangu, kuna muda nahofu

Oooh nakumbuka wana wa Israeli
Katika bahari la shamu
Japo walikatiza 
Katikati ya bahari kwa ushindi

Kwa nyimbo nyingi
Waliimba na kumsifu Bwana
Lakini baada ya kuvuka na kuliona jangwa
Yalibadilika mambo

Manung'uniko yalisimama aah
Na kusahau muujiza alotenda bwana mwanzo
Aaah...
Eeeh Mungu nisaidie eeh eeh eeh, oooh

Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa magumu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu

Niimbe wimbo wa sifa
Katikati ya machozi
Niimbe wimbo wa sifa
Katikati ya machozi eeh eh

Eh Mungu nisaidie 

Nisaidie kukumbuka Baba
Ya kwamba umenichora kiganjani mwako
Kati ya wengi waliopo duniani 
Na mimi umeniona oooh..

Nikumbushe bwana kwamba ni wewe
Unaniponya ninapoumwa
Kwamba ni wewe 
Mlipaji wa ada yangu shuleni oooh..

Yakwamba kama umeniacha hatua moja
Nisingelifika mahali nilipo
Eeeh Baba, umeniukung'uta mavumbi
Kung'uta mavumbi mimi na kuniheshimisha oooh..

Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa magumu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu

Niimbe wimbo wa sifa
Katikati ya machozi
Niimbe wimbo wa sifa
Katikati ya machozi eeh eh

Leave a Comment