Wajinga Sisi Lyrics
Wajinga Sisi Lyrics by FRASHA
Hello, Hello! King Kaka, ni Frasha hapa
Manze hii fight alone hauwezi toboa
So nimeamua kustand na wewe
So kabla wani-surmone wacha nitoe yangu surmone
Naskia Waiguru amekusue, is this true?
Funny vile judiciary imekuwa circus
Judge na politicians wakiwa main acts
Mshukiwa anaachiliwa kwa bondi ya milioni mbili
Na kesi yake ni ya bilioni mbili
Nani atatupigania?
Hatujui maguru wa NYS
Na Ruto na makesi za mashamba scandal za mahindi
Na story za Mumias na sukari
Na ata kama we ni pastor unang'ang'anana
How can you have a deceitful tongue?
But Sunday church bado tutajazana
Wajinga Sisi!
Story ya SGR tuliacha kujicompare na Ethiopia
Wale pia walikuwa wanapiga kelele walinyamazishwa
Pia 'hello unanskia?'
System ya education ni ya kubebesha punda mzigo
Hapo ndo mwanzao wa mitego
We go to schools to become educated fools with no jobs
Justice ni ya wenye doh
Lawyers nao ni beneficiaries of failed system
No wonder masomo inaitagwa system, Wajinga Sisi!
Na ata kama wakitumada
Damu ya Sharon bado Inatu-owe bado
Siogopi kufa juu kwa system niko dead
Na bado me si sonko
Na hakutakuwa na commission of inquiries
Wasee wapate makazi na salary
No wonder bado vijana wako moody daily
Wakiworry hii kesho itafika lini
Juu bado si ni wazee na ni future leaders
Hello, Hello, mnanisikia? Wajinga Sisi!
Daily tuko kwa mitandao IG na Twitter
Tukionesha venye tunaishi poa
Ni kama kila mtu alitoboa
Picha kwenye hoteli na meli daily
But ukweli tuko chini tunasuffer
Vitu hard kwenye ground
Kwenye matanga hakuna mtu ako sad
Familia ikilia wanasiasa wanaji campaign-ia
nimesaidia familia na elfu mia
Kisha makofi tunawapigia
Wajinga Sisi!
Itaanza kutuuma lini sisi?
Itaanza kutusumbua lini sisi?
Future generations ni kina nani?
Na nani watawapigania
Tunashinda tukipuliza gunia
Eeeh Mungu nguvu yetu
Ilete baraka kwetu
Haki iwe ngao na mlinzi
Na tukae na undugu, amani na uhuru
Bado kuwa mkenya najivunia
But nimechoka kuvumilia
Time ni ya kujipigania
Tokeni mitandaoni
Kujeni tujenge Kenya
Maovu ni maovu
Haijalishi ni nani aliyatenda
Na sitasimama maovu yakitawala
Wakiuza sura badala ya kuuza sera
Ju hand-outs hazitawai kujengea barabara
Hand-outs hazitawai kujengea shule
Hand-outs ndio kabila ya umasikini
Hallo!
Watch Video
About Wajinga Sisi
More FRASHA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl