
Paroles de Nimevuka
...
Paroles de Nimevuka Par TOXIC
Kipindi ambacho namuhitaji kuliko chochote
Ndio kipindi ambacho aliondokaga
Nikafanya kila juhudi ili asiondoke
Lakini bado akaondokaga
Na sikuwahi kumcheat wala kumuumiza
Nilijenga uaminifu hadi ikafikiaga
Niliposema nina mpenzi alijijua ni yeye tu
Hata jina lake nisipolitaja
Mapenzi sio utamu ila uchizi
Mapenzi na kupumzika haviendani vitu hivi
Ndio maana yakinoga wachlewesha kulala
Yakianza kuisha ndio kabisa yankunyima usingizi
Imani yangu iliniambia iwapo nitamwacha aondoke
Kama yeye sitampata bara na visiwani kote
Hivyo uwoga wangu wa kumpoteza
Ukanifanya ninyamaze
Hata vitu ambavyo nilitakiwa niropoke
Sikuzama deep tu, niliingia mpaka ndani ya udongo
Hapondio moyo ulianza kuongoza ubongo
Maumivu yake yakanifanya niamini
Nyimbo zote zinazosifia mapenzi ni za uongo
Unaona bonde unselezwa huu ni mlima
Sikuwa mjinga ila niliuchagua ukimya
Kwakuwa niliongozwa na mapenzi
Hivyo niliukubali uwongo
Ambao hauwezi ukamdanganya mtu mzima
Pengine sijui what’s the meaning of love
Na matatizo ya fedha halafu
Sina hata kumi mbovu
Kipindi ambacho nilimuhitaji anifariji
Nae aligeuka kuwa tatizo nilotakiwa kulisolve
Yaani stress za mapenzi kuna kiwango ukivuka
Sometime anakuwa hafarijiwi
Hata na watu wanaomzunguka
Unajimix na washikaji ilimradi umsahau
Unawasahau hao washikaji
Ila yeye ndio unamkumbuka
Jambo ambalo utagundua akili ikiwa na utulivu
Sio kila aliye juu ana mentality za uvivu
Kuna muda unapitia magumu
Ambayo kifo ndio kina kuwa njia pekee ya kutuliza maumivu
Ecouter
A Propos de "Nimevuka"
Plus de Lyrics de TOXIC
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Vous aimeriez sûrement
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl