Paroles de Zibambwe
Paroles de Zibambwe Par ROMA
Tongwe records
Bin laden (Oooooh)
Geof Master (ooooh)
Wengi mlijiuliza walioniteka ni maaskari
Mkanitafuta vituo vyote Central hadi Sitaki Shari
Wakasema hawajui nilipo mama alienda hadi mortuary
Dah! Ya Kaisari muachie Kaisari
Machozi yenu yatalipwa
Mi nafunga na kusali
Imba Roma imba, imba Roma imba
Imba Roma imba
Mungu wa Paulo, ndo Mungu ungu wa Daudi
Na ndo Mungu wa John mnaemuita Yohana wa Yahudi
Mwanangu alimuuliza mama baba lini atarudi
Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru sina budi
Fahamu ya kuwa mi sio tu rappa, mi ni baba wa familia
Na watoto mahitaji nawapa kama isemavyo Biblia
Kipi bora? Nife mseme nilikufa kiharakati?
Siogopi kufa, ila nawaachaje wanaobaki?
Je, nani kati yenu mwanangu atampa malezi?
Wapi atapata mahitaji, wapi atapata mapenzi?
Mama nae wapi atapata mahitaji na malezi?
Na ripoti ya upelelezi vipi akiiteka mtekaji?
Je kaburi langu mtalipalilia majani?
Nimeumwa hamjakuja niona mnangoja mje msibani
Nilipokuwepo sikuwa najua hii saa nne, hii saa nane
Nilichohitaji nitoke mzima na ndugu zangu tuonane
Nimechapwa mijeledi, nimevunjwa bila huruma
Asante mliopaza sauti nmeiona nguvu ya umma
Siku tatu nimefungwa macho
Mikono imefungwa nyuma (Mikono imefungwa nyuma)
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee
Imba Roma imbaaa (oooh)
Eeeh Roma, sema baba weeeh
Nasimama na naunga hoja kwenye uchumi wa viwanda
Nanasi linaoza mzoga tikiti linaoza shamba
Waloniteka hawakuja na Noah, ni uvumi na visanga
Ila kutekana tekana huu ni uhuni wa kishamba
Weka bunduki chini si tubishane kwa hoja
Maana sote lengo letu kuijenga Tanzania moja
Mi sikuona nyota kwa shoulder ila najua we ni soldier
Inshaallah, ulikuja mwenyewe ama ulipewa order?
Aminini siku hazigandi
We ni Yanga mi Simba kuwa mpinzani sio dhambi
Ipo siku mtawala atakua mpinzani
Simba akichukia kombe sijui atapona nani?
Na kuna mbunge alisema eti nimemtukana mkuu
Utahukumiwa na mkono wa Mungu, namshitakia alie juu
Kwanza lini na kwaninii nimtukane mjomba?
Umepewa gari ya wagonjwa mi Tanga ananijengea bomba
Mi mbarikiwa na nikifa kuume kwa baba ntaketi
Na mtu wa watu that's why lilisimama bunge la bajeti
Kunijadili mtanzania kuwa makini pia
Makinikia nayatungia mapini pia
Nilitabiri utaitwa raisi kipindi unaitwa waziri
Japo maisha sio rahisi ila pongezi unastahili
Na waliosadiki Roma ataonekana kabla ya Jumapili
God bless imetimia injiri niliyoitabiri
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee
Imba Roma
Eeeeeeh Roma, simama simama
Oyoyoyo eeeeeh Roma
Sema baba wee
Iyelele mama wee, wee nakwenda
Wee Zimbabwe
Iyelele mama wee, mama wee
Ooooh
Ecouter
A Propos de "Zibambwe"
Plus de Lyrics de ROMA
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Vous aimeriez sûrement
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl