Paroles de Maneno
Paroles de Maneno Par REBEKAH DAWN
Wakati mwingine
Nikiketi kukuimbia mie
Huwa nalemewa
Kupata maneno yanayoshimiri
Ni kama mtoto mchanga anapojaribu
Kueleza ukubwa wa sayari
Ni kama kidege kinapojaribu
Kueleza upana wa mbingu
Ni kama changarawe kujaribu
Kueleza ukubwa wa bahari
Ukweli ni kwamba
Maneno yangu hayatoshi
Hayawezi kueleza
Hivyo daima na milele
Siku zote za maisha yangu
Nitatafuta kukuimbia
maneno yanayokufaa
Wakati mwingine
Nikiketi kukuimbia mie
Huwa nalemewa
Kupata maneno yanayoshimiri
Ni kama tone la maji
Kujaribu kueleza mfuriko wa mvua
Ni kama wapendanao
Kujaribu kueleza fumbo la penzi
Ni kama mshumaa kujaribu
Kueleza kung’aa kwa jua
Ukweli ni kwamba
Maneno yangu hayatoshi
Hayawezi kueleza
Hivyo daima na milele
Siku zote za maisha yangu
Nitatafuta kukuimbia
Maneno yanayokufaa
Ni kama jiwe linapojaribu
Kueleza urefu wa mlima
Ni kama sheha shupavu kujaribu
Kueleza hadithi zote za jadi
Ni kama mwenye dhambi kujaribu
Kueleza neema ya msamaha
Ukweli ni kwamba
Maneno yangu hayatoshi
Hayawezi kueleza
Hivyo daima na milele
Siku zote za maisha yangu
Nitatafuta kukuimbia
Maneno yanayokufaa
Ecouter
A Propos de "Maneno"
Plus de Lyrics de REBEKAH DAWN
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl