MALKIA KAREN  Nishazoea cover image

Paroles de Nishazoea

Paroles de Nishazoea Par MALKIA KAREN


Nderemooo
Na vifijo si mayowe
Te amo, furaha yangu kupendwa na wewe
Maneno wasemayo na yapuza ujue
Sikurushi roho
Nikuache uume
Na sina sifa ya kuku
Kila da ni nipakue mie
Wala lopo ya kasubu
Ya watu niyahadithie
Upole wangu tausi
Vicengeni hunikuti
Na sina huba la nuksi
Nakshi zangu ni marashi

Sawa
Kusemwa nishazoea
Haya
Mwenzako nishazoea
Sawa
Kusemwa nishazoea
Haya
Mwenzako nishazoea

Mi sitowaa vimini
Vya mpasuo kwetu mwiko
Natinga baibui mwilini na
Videra vya baikoko
Tena najitia uturi
Viyasmini vya mtoko
Nikupeleke nyumbani
Kisiwa cha karafuu
Tukale madoriani
Shoko shoko za udambu
Jioni twende forodhani
Tukale upepo mwanana
Chaza mchukue mwambani
Na iwe zawadi ya mama
Upole wangu tausi
Vigengeni hunikuti
Na sina huba la nuksi
Nakshi zangu ni marashi

Sawa
Kusemwa nishazoea
Haya
Mwenzako nishazoea
Sawa
Kusemwa nishazoea
Haya
Mwenzako nishazoea

Ecouter

A Propos de "Nishazoea"

Album : Nishazoea (Single)
Année de Sortie : 2022
Ajouté par : Farida
Published : Oct 06 , 2022

Plus de Lyrics de MALKIA KAREN

MALKIA KAREN
MALKIA KAREN
MALKIA KAREN
MALKIA KAREN

Commentaires ( 0 )

Aucun commentaire pour l'instant



A propos de AfrikaLyrics

Afrika Lyrics est la plus large collection de paroles de chansons et de traductions d’Afrique. Afrika Lyrics fournit les paroles des musiques de plus de 30 pays africains et des traductions de lyrics de plus de 10 langues africaines en français et en anglais.

Suivre Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl