Paroles de Corona
Paroles de Corona Par BEKA FLAVOUR
(Mafia)
Hili gonjwa ni hatari
Na tena linaua, ua
Ni tishio duniani
Nani asiyejua, jua
Kusema za ukweli Corona ni pigo
Mpaka sasa dawa haijulikani bado
Tujilinde wenyewe kwa hili tatizo
Tusipeane mikono chonde chonde
Safari zisomuhimu tusiende
Tuvae mask chafia tuzikinge
Ndio kinga mbadala aah
Mabusu kupigana vyama tusipende
Ili tusiambukizane tujikinge
Mpaka gonjwa hili lipite
Tuombe Mungu atunusuru kwa hili
Tusichukulie tu poa poa
Corona gonjwa hatari
Watu wanakwisha
Nchi zote duniani
Tusichukulie tu poa poa
Corona gonjwa hatari
Watu wanakwisha
Nchi zote duniani
Na serikali inatupenda
Ndio maana wamezifunga shule
Mikutano ya kisiasa yote wameitupa kule
Na matamasha wasanii hakuna kule
Wangeruhusu yaani ingekuwa sawasawa na bure
Tunawe mikono kwa maji safi salama
Sanitizer nyumbani no kukosekana
Salamu mbali mbali no Kugusana
Aaaa aaah...
Tusipeane mikono chonde chonde
Safari zisomuhimu tusiende
Tuvae mask chafia tuzikinge
Ndio kinga mbadala aah
Mabusu kupigana vyama tusipende
Ili tusiambukizane tujikinge
Mpaka gonjwa hili lipite
Tuombe Mungu atunusuru kwa hili
Tusichukulie tu poa poa
Corona gonjwa hatari
Watu wanakwisha
Nchi zote duniani
Tusichukulie tu poa poa
Corona gonjwa hatari
Watu wanakufa eh
Nchi zote duniani
Bado tunakuomba Mungu Baba
Utunusuru na hili janga
Rais wetu Magufuli baba
Umnusuru na hili janga
Bado tunakuomba Mungu Baba
Utunusuru na hili janga
Ommy mwalimu ooh mama
Umnusuru na hili janga
Bado mi nakuomba Mungu Baba
Uninusuru na hili janga
Mwanangu Ariani
Umnusuru na hili janga eh
Ooh Tanzania
Utunusuru na hili janga
(Mafia)
Ecouter
A Propos de "Corona"
Plus de Lyrics de BEKA FLAVOUR
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Vous aimeriez sûrement
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl