
Nalia Lyrics
Nalia Lyrics by FEROOZ
Ukiona mtu mzima analia
Ujue kuna jambo limemsibu
Nimeshindwa kuvumilia
Moyo umepatwa na ghadhabu
Kama tatizo fedha rushwa ningekutolea
Ama ningeweza dhamana ningekuwekea
Lakini imeshindikana chini ya jua
Kama usingizi mauti amekuchukua
Halaumiwi Maulana
Ye anakupenda sana
Kapumzike salama
Kesho tutaonana tena
Hakikwepeki kifo mama
Naamini siku ipo tutaonana
Kifo hakina mwiko wala ujamaa
Na sote tutakwenda kwa Maulana
Kiza kimetanda mwanga mshumaa
Huzuni imetawala furaha imesinya
Nalia kutoka moyoni
Kukuona tena natamani
Nakuchomea na ubani
Mola akulaze peponi
Nalia kutoka moyoni
Kukuona tena natamani
Nakuchomea na ubani
Mola akulaze peponi
Ndo ameshalala huyo haamki
Hata mmshikie bunduki hatokaa
Hatwafaa, ila roho yake itapaa
Ndo maandiko yanavyosema
Maana huwezi tena kwema
Japo ametuacha mapema dah
Sasa amkeni muageni
Mumpe heshima za mwisho
Maana hamtomuona tena
Na pia mpate fundisho
Hiki ni kifo sio sinema
Na aliyezaliwa na mwanamke
Siku zake zinakwisha
Sasa basi sote tuinuke
Tujiandae kwenda kumzika
Loka ashaingizwa kwenye mwandani
Na si tushauchoma ubani
Basi turudi nyumbani
Huku tukitafakari baada ya ye atafuata nani
Labda wewe
Basi swali usingoje uswaliwe na watu
Kaburini utakuwa mwenyewe
Ukiongoja malaika wa wafu
Nanyi mnaoshika chepe
Kumfukia mwenzenu
Siku nanyi mtafikiwa itakapokata pumzi yenu
Sasa msisite msiogope
Mkaacha kumzika mwamba mkachimba
Mbinguni hauingiii na kope
Sasa iweje unavimba
Unadharau wenzako
Kwa jeuri ya madaraka
Na kwa kiburi cha cheo
Unawatoa wenzio sadaka
Kwa umaarufu wako wa leo
Unatuona si taka taka
Kwa pesa zako na mkeo
Unakosa utu unanata
Haya si ulimchukia marehemu
Leo hayupo tena duniani
Unatamani aamke umuombe msamaha
Na haiwezekani
Ikiwa umezaliwa makongo
Ukipinga kifo hauwezi
Sote tutarudi kwenye udongo
Kiza kimetanda mwanga mshumaa
Huzuni imetawala furaha imesinya
Nalia kutoka moyoni
Kukuona tena natamani
Nakuchomea na ubani
Mola akulaze peponi
Nalia kutoka moyoni
Kukuona tena natamani
Nakuchomea na ubani
Mola akulaze peponi
Watch Video
About Nalia
More FEROOZ Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl