ECHO  Nimekubali cover image

Nimekubali Lyrics

Nimekubali Lyrics by ECHO


Barua yako uliyonitumia nimeisoma
Ila kiukweli sijafurahia
Ata na moyoni imenichoma iyee iyee
Mi ndo niliyekuwa wa kukuchoma
Leo dunia inanizoma
Kiraka mi ndo niliyekishona
Leo kimepata mwenyewe kikanipokonya

Nilikuwa domo zege wakati ule
Ule ule ule ule
Nilizama mani baby leta tule
Tule tule tule tule

Nitaufosi moyo ukubali
Ila ujue tumetoka mbali
Natamani ningerudi awali
Hata mi ningeliuliza swali

Nitaufosi moyo ukubali
Ila ujue tumetoka mbali
Natamani ningerudi awali
Hata mi ningeliuliza swali

Nimekubali, nimekubali
Japo kishingo upande
Nimekubali, nimekubali
Nimeruhusu uende

Nimekubali, nimekubali
Japo kishingo upande
Nimekubali, nimekubali
Nimeruhusu uende

Nahisi labda haikuwa bahati yangu
Huenda hukupangwa kuwa wangu
Ila nilikupa kilicho changu
Umelizika lengo langu

Laiti ningejua
Kwa mapenzi mi vita ningezama ulingoni
Moyo unaumia
Nikitazama picha tulopiga udogoni

Mmmh kwenye harusi yako nitahudhuria
Na vizawadi nitakuletea
Unataka nyimbo nitakuimbia, aah aah aah

kwenye harusi yako nitahudhuria
Na vizawadi nitakuletea
Nataka nyimbo nitakuimbia, aah aah aah

Nimekubali, nimekubali
Japo kishingo upande
Nimekubali, nimekubali
Nimeruhusu uende

Nimekubali, nimekubali
Japo kishingo upande
Nimekubali, nimekubali
Nimeruhusu uende

Watch Video

About Nimekubali

Album : Nimekubali (Single)
Release Year : 2021
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
Published : Aug 16 , 2021

More ECHO Lyrics

ECHO
ECHO
ECHO
ECHO

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl