Ujana Lyrics

ASALA Feat TUNDA MAN Tanzanie | Bongo Flava,

Ujana Lyrics


Kweli mapenzi ushujaa 
Vita ni kupambana
Yule anaye kupenda sana
Ndo utamuona yeye ana maana

Ngoja nikwambie
Kupendwa bahati wanatafuta wenzako
Tena usikie
Hairudi mara mbili tumia nafasi yako

Nafsi imejawa tamaa
Macho yanakutazama
Vyomoni nakupenda sana 
Kumbe moyoni nakudanganya

Tatizo lako wewe
Kila kitu unakitaka wewe
Dunia ina wengi we
Hutaweza kumaliza utamu wee

Kila kukicha nafadhaika 
Kaka eeh
Moyo hutaki ridhika
Mpaka nimpate Wema eeh

We mwana ukome tena domo lishone
Naona kama unavuka mipaka
Usijidanganye na usijichanganye
Kashindwa simba utaweza wewe paka

Si unajuaga ujana
Una mambo mengi ujana
Chunga sana ujana
Ni maji ya moto ujana

Nasema si unajuaga ujana
Unafanya nisilale ujana
Utalia ujana
Utakupoteza ujana

Mapenzi starehe yangu
Kuwacha siwezi aiyaa
Nazunguka na moyo wangu
Ila pesa ndo nawagawia

Anacheza na akili yako
Ana nguvu sana huyo shetani
Tafuta chaguo lako
Umveshe pete umweke ndani

Dunia ya leo,
Maradhi yako wazi wazi
Achana na vileo
Umaarufu usikupe uchizi

Kila kukicha nafadhaika 
Kaka eeh
Moyo hutaki ridhika
Mpaka nimpate Wema eeh

We mwana ukome tena domo lishone
Naona kama unavuka mipaka
Usijidanganye na usijichanganye
Kashindwa simba utaweza wewe paka

Si unajuaga ujana
Una mambo mengi ujana
Chunga sana ujana
Ni maji ya moto ujana

Nasema si unajuaga ujana
Unafanya nisilale ujana
Utalia ujana
Utakupoteza ujana

Big Sound Music

Leave a Comment