Mawaidha Lyrics
Mawaidha Lyrics by MAARIFA
Naitwa Maarifa ila baba ananiita Rashid
Eti wanaitika ila ibada imeniita zaid
Inaniita Zaid naitika kwa ujenzi wa tungo
Nawakumbusha tumefika mwezi wa mfungo
Sali toa sadaka skia usijejikweza
Soma Kurani kisha saidia wasiojiweza
Kuelewa hiari siwezi chukia ukija nibeza
Ila fahamu hakuna kujibebea jeneza
Ikiingia hasara huwa ishara lahaula
Hivi unaskia na pia nakwambia
Hata kusoma hadith kula mshahara wa nusura
Hadithi za mtume sio za Kajala na Paula
Sio tu kungata tu zaidi haupulizi
Unasahau sala ni bora zaidi ya usingizi
Zaidi haulizi hata ukiumia juu nakuponda
Ukitaka kuwa nzi jiandae kufia juu ya kidonda
Ukiskia zana kwa maaana, chunga
Hata ka ulikuwa unapambana, funga
Hata kama ulikuwa na uhasama, vunga
Kwa sasa kitu cha maana, funga
Nafsi na mwili yaani ni zaidi ya kula na kunywa
Ya mimi mimi nazi fuliwa kabla ya kukunwa
Kabla ya ku, ya kukupa nguvu mi haunidhibiti
Aliyekupa we mshumaa alinipa mie kiberiti
He lifts me high and I spread my wings
Fly me to the sky now I am doing my things
I'm doing my thing na wema wake ninahadithia
Sitazami vyote japo macho hayana pazia
Ah mtu mmoja sina wazimu, sina wazimu mtu mmoja
Mungu mmoja sina team, sina team Mungu mmoja
Tuombe msamaha hata kwa magumu ya kaburi
Ramadhan kareem saum makubuli (Amen)
Tuzingatie moja moja ya mafungu (Amen)
Tusiaminie ngoja ngoja kwa utundu (Amen)
Niamini mie na hizi hoja kwa uchungu
Si eti Mungu awe nasi tuwe pamoja na Mungu (Amen)
Watch Video
About Mawaidha
More MAARIFA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl