Wewe Lyrics by KALA JEREMIAH


Nisikilize mimi kama unataka uolewe
Kabla ya kupenda hakikisha unajipenda mwenyewe
Naongea na wewe
Puuza haya maandiko kama mpira uchezewe

We kifaranga cheki juu kuna wingu la mwewe
Wanasubiri ujichanganye, ubugi, upitiwe
Usifiwe sifiwe udanganywe uchachuliwe
Kama makinikia zubaa uchenjuliwe

Keusi kekundu funika kisha ufunuliwe
Weka tamaa mbele ka kuku ununuliwe
Udanganyike kwa mtama uchinjwe uliwe
Kuwa makini kutofautisha mwamba na jiwe

Akikupenda muende angaza mpime ndo uolewe
Usikubali kuwa mjinga binti mzuri kama wewe
Punguza kiwewe
Akikutoa out usikubali ulewe
Hata nauli ya bajaji usikubali upewe
Na ukifuata niyasemayo haitatokea uchezewe
 
Nasema nasema nasema nasema na wewe dada
Usijifanye hunisikii naongea na wewe
(Usijifanye hunisikii naongea na wewe
Naanza na wewe na mwingine anafuatia
(usijifanye hunisikii naongea na wewe
Usijifanye hunisikii mi naongea na wewe wewe
Naongea na wewe wewe
Naongea na wewe wewe
Naongea na wewe wewe

Umeolewa uko nyumbani mume ametoka
Shati na suruali hakikisha vimenyooka
Usisahau kujifunza kung'arisha moka
Akirudi mpe kiss hata kama ni mtu wa kumoka
Akitaka umpe mpe hata kama umechoka
Kesheni macho mtalala uzeeni kama choka
We ndo mwanamke wa shoka

La liga ikianza kaa nae mcheki soccer
Muulize mesi ndo yupi? Hata kama unamnyaka
Yani listen mama please say mama 
Kama una sifa hizi sema uko wapi?
Niko njiani sema nikufuate wapi?

Yoooh nina maswali kichwani
Je utafia msibani? Au utafia vitani?
Je utaweza kuyashinda majaribu ya shetani
Au utaishia njiani kisa neno la jirani?
Umtupe mkono mwenzako umchinje nyani
Upendo wa mwenzako ugeuke rungu kichwani
Umtoboe macho kisha umsukumize gizani?

Nasema nasema nasema nasema na wewe dada
Usijifanye hunisikii naongea na wewe
(Usijifanye hunisikii naongea na wewe)
Naanza na wewe na mwingine anafuatia
(Usijifanye hunisikii naongea na wewe)
Usijifanye hunisikii mi naongea na wewe wewe
Naongea na wewe wewe
Naongea na wewe wewe
Naongea na wewe wewe

Ndoa ina mambo kibao
Kaa mbali na simu ya mwenza na mitandao
Waepuke rafiki vishungi na vichwa vyao
Waambie mapema wafunge bakuli zao
Karibu na mume wako wasisogeze kwato zao
Ni kufa ama kupona zubaa upigwe bao
Wanataka usimame kwa kiti wakae wao
Kufa na chako waambie wakafie makwao
Umependeza wao

Mungu awape baraka za mifugo na mazao
Awape afya bora kisha awape uzao
Chini ya paa kukuruka mpaka aombe po
Kama unalipwa doh
Jasho mwili mzima ile level ya kukata roho
Kaka akizinduka ataimba ile verse ya milupo noooo
Yooh 0444

Hatariiii lakini salama
Jamanii we boss kalewa leo
Wanangu boss kalewa leo
Wanangu wana beli kali 
Wanadundo kali wana bamba kali wanangu wanawakaaa

Wanameremeta wanawaka
Wanangu wanameremeta wanawakaa
Masela boss kalewa leoo
Basi tena nipe tena

Watch Video

About Wewe

Album : Wewe (Single)
Release Year : 2021
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
Published : Feb 12 , 2021

More KALA JEREMIAH Lyrics

KALA JEREMIAH
KALA JEREMIAH
KALA JEREMIAH
KALA JEREMIAH

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl