
Dunia Lyrics
...
Dunia Lyrics by HANSTONE
Mi mwenyewe mtoto, mi ningali motto
Nakinga jahazi lisije kuzama maana maji ya ugoko
Nyingi changamoto, kuifikia ndoto
Najichunga nisije ungua, na ujana maji ya moto
Hata ujipange dunia (dunia), nani alikuambia?
Naomba uyasikie siku ya mwisho, wanayosema hata usiowadhania
Utacheka, utalia. Haina mzani dunia
Wapo wanaoomba uteseke. (Aaaaah aaah)
Kasema baba nsifuate dunia
Aliniambia mama nisifuate dunia (Aaaah)
Alisema bibi kaiacha dunia
Na wewe utasema utaiaga dunia (Ooooh)
Jamani dunia. Ooooh dunia. Aaaah dunia
Ooooh dunia. Lisemwa. Lisemwa (Oh)
Lisemwalo lipo, kama halipo basi laja
Yalisemwa (Oooh). Yalinenwa (Oh)
Yanapozidi mateso, inakuja faraja (Aaaaah)
Oh, eti dunia duara
Kuna muda kama siamini
Naona kama imenyooka, tunapokwenda twaishia chini
Jamvi na mswala, turudi kwetu tunayemuamini
Usishangae rafiki anakua adui, kwa sababu ya aliye akilini (Mmmh)
Mwenye anacho, ambaye hana hathaminiki
Kwa tumachomacho, kwa kubaniana riziki
Kikulacho kinatafuna hata mbichimbichi
Yaani dunia bado hata ukilia haisaidii (Aaaaaaah aaaaaah)
Kasema baba nsifuate dunia
Aliniambia mama nsifuate dunia
Alisema bibi kaiacha dunia
Nawe utasema utaiaga dunia (Ooooh)
Chuki, chuki inaanzaga kwa upendo (Mmmh)
Mamluki watakusemasema sio matendo
Sa sijui, nimuamini yupi?
Yupi nimkabidhi upendo
Moyo wangu asije dilute, akanichanganya, waniroge, aniachie pengo. (Aah)
Dunia pana, dunia tambara bovu. Sijui ndo mwisho
Maulana, yanazidi maovu
Watu wanashindana kufanya michezo mibovu
Au hata kuhakikisha kidonda linabaki kovu
Aaah, dunia. Ooooh, dunia. Mmmh. Mmmh
Kupata mpaka uwe na roho mbaya, ndivyo 'navyosema
Hata Mungu pia hafundishi ubaya, wanautoa wapi tena?
Tisa mzuri ila moja baya, wanafuta yote mema
Wanaomba kuzaliwa mbwa ulaya, sio kujiombea mahali pema
Kwa wanadam, Mungu tukumbushe
Kama dunia safar, njiani unishushe
Oh baba, nami univushe
Na ya dunia ni majaribu, naomba uniepushe (Aaah)
Watch Video
About Dunia
More HANSTONE Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl