Utamu Lyrics by HAITHAM KIM


Tumeenda Nyota 
Visura vyetu kama Mapacha
Ukingoni nishagota 
Yani utamu kama bazooka 

Navunja milango ya usaliti 
Baby we unanitosha 
Samaki mkunje angali mbichi 
Kwako sina ninachokosa 

Penzi lako mneso nabembea (Bembeaa)
Sunche mi kapeto nshakoleaa 
Tukiwaga ghetto nalegea (Legeaa)
Ukisema kesho nangojea 

Kwako kilema Bila gongo sitembei
Thamani ya genge huwa ni bei
Mi kimyaa tena bubu siongei 
Umenikata ngebe sina sei 

Kama Penzi lako ni maji ni maji 
Basi Leo mi ntaogelea 
Na kama penzi lako midadi midadi 
Basi utamu mi ndo ushan'nogea 

Ushan'nogea ushan'nogea (Utamu)
Ushan'kolea  Ushan'kolea (Utamu)
Ushan'nogea utamu ushan'nogea (Utamu)
Ushan'kolea  Ushan'kolea (Utamu)

Utamu u-utamu utamu 
Utamu ushan'kolea ushanikolea

Wapi unataka nikupeleke Sema 
Mtihani wa mahaba nakupa zote vyema
Kutwa unacheka hata nisipo kutekenya
Unanipa nnachosema nitake nini 

Tena zaidi ya utamu   
Mtu chake bwana mi napata utamu 
Kasura kako ka kitoto kamekaa utamu
Sura ina haya imechanganyika na tabasamu 

Na hizi Corona ndani tu nakulamba utamu
Niwazi nimekufa nimeoza 
Pongezi namtumia mama mzazi aliye kuzaa
Wakisema haupendezi haushindani kuvaa
Wana kitaani wanasema nimeokota kifaa

(Ndio ndio)

Nisipo kuona moyo unakwenda mbio mbio 
Ndani ya moyo wangu uko peke yako ndio ndio 
Maneno ya wanga fanya kuyazibia masikio 
Wataacha tu au sio, kuachana hiyo kwioo

Kama Penzi lako ni maji ni maji 
Basi Leo mi ntaogelea 
Na kama penzi lako midadi midadi 
Basi utamu mi ndo ushan'nogea 

Ushan'nogea ushan'nogea (Utamu)
Ushan'kolea  Ushan'kolea (Utamu)
Ushan'nogea utamu ushan'nogea (Utamu)
Ushan'kolea  Ushan'kolea (Utamu)

Utamu u-utamu utamu 
Utamu ushan'kolea ushanikolea

Watch Video

About Utamu

Album : Utamu (Single)
Release Year : 2020
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jul 14 , 2020

More HAITHAM KIM Lyrics

HAITHAM KIM
HAITHAM KIM
HAITHAM KIM
HAITHAM KIM

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl