BARNABA Bado Muda cover image

Bado Muda Lyrics

Bado Muda Lyrics by BARNABA


Eeeh ayooo ahh nanana...
Usilie machozi ungali bado unapumua
Usikufuru Mungu ungali hii sauti unasikia
Wewe umepanga milioni yeye amepanga sufuri
Wewe umepanga ghorofa
Yeye amepanga kibanda
Ulipanga ule nyama kesho kesho unakula dagaa
Usikate tamaa bado una mudaa
Shetani hakosi kushindwa
Bado na muda
Ayoooo oo

Mwenzako kalala mochwari hajitambui
Hajui nani anapita
Nani anamwita nani anaingia
Wewe unaona na unashuhudia
Bado una muda
Aaah eeh...  bado una muda

Mwaka unakatika ulipanga ujenge ghorofa
Mwaka unakatika ulipanga ununue verosa
Alhamdulilahi umeambulia baiskeli
Wakati mwenzako kavuna kwenye mwaka ukilema
Si unapumua angali mzima
Bado una muda

Shetani alimjaribu Ayubu
Kwa kumpanga majaribu
Alimpaka upele mwili mzima

Mke wa Ayubu akasema Ayubu ananuka
Ayubu alishinda mitihani
We je wewe, bado una muda

[CHORUS]
Usilalame usitukane zidi kupambana
Mungu anaona, muda wako waja atakugusa
Ukikosa leo usikufuru Mungu
The time has come
Usilalame usitukane zidi kupambana
Mungu anaona, muda wako waja atakugusa
Ooooh ooooh oohh...

Mama nitilie unasema Mungu kakuonea
Ewe beba Segel unasema Mungu kapendelea
Wakati una mikono
Kakubariki na macho na masikio
Kuna mwingine hasikii kabisa
Kuna mwingine hatembei kabisa
Heri kutembea
Kuna mwingine hashiki kabisa
Wewe unapata nguvu kushika mikono
Bado una muda
Aaah bado una muda

Sauti hii kama unasikia
Sikia timamu
Sikia timamu na ufahamu
Kama unatambua ninachozungumza
Bado una muda, aaah bado una muda

Mungu ametenda mengi juu yangu(mmmh)
Kuna muda niliachwa na Baba na Mama
Hadi mpaka na wife (na wife)
Yeye hakunitupa (aaah aaah)
Alininyenyua, akanitembeza
Akanishika mkono
Akanionyesha mahali sahihi
Natabasamu nina muda

Mwingine anaoa leo kesho anaacha
Mwingine anaolewa leo kesho anaachwa
Wewe umedumu kwenye ndoa furahi bado una muda
Usiache kumuomba yeye bado una muda

Wewe umeolewa jana leo umepigwa
Wewe umeoa jana leo umesalitiwa
Usilalame bado una muda

In the name of Jesus Jesus bado una muda
In the name of the Lord of the mass bado una muda
In the name of God Messiah bado una muda
In the name of Yudah wa Yudah....
Ananguruma you got time

Usilalame usitukane zidi kupambana
Mungu anaona, muda wako waja atakugusa
Ukikosa leo usikufuru Mungu
The time has come

Usilalame usitukane zidi kupambana
Mungu anaona, muda wako waja atakugusa
Ooooh ooooh oohh...

Naimba kwa sababu yake yeye
Bado una muda....

 

Watch Video

About Bado Muda

Album : Asante (EP)
Release Year : 0
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jan 05 , 2019

More BARNABA Lyrics

BARNABA
BARNABA
BARNABA
BARNABA

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl