Utoshefu Lyrics
Utoshefu Lyrics by AMBWENE MWASONGWE
Nimejifunza kuwa radhi, katika hali yeyote niliyonayo
Najua kudhiriwa, tena na kufanikiwa katika hali yeyote
Na katika mambo yeyote nimejifunza kushiba na kuona njaa
Nimejifunza kuwa na vingi na kupungukiwa, nayaweza yote kwa anitiaye nguvu
Utauwa, na kuridhika vimenipa utoshefu
Utauwa, na kuridhika vimenipa utoshefu
Furahini siku zote katika bwana
Tena nasema ndugu zangu furahini
Upole wenu ujulikane na watu wote
Bwana yu karibu kuja
Furaha niliyonayo, ni tunda la roho furaha hiyo hailetwi na vitu
Sisubiri nipewe ili nifurahi, nafurahi hata kwenye mateso
Upole nilionao, umetoka kwa roho hautegemei ninavyotendewa
Amani ya Kristo imenitawala ndani naimba wimbo wakati wa shida
Imenihifadhi moyo na nia yangu ninayapenda mambo ya staha
Haki, usafi kupendeza na sifa njema
Ukiwepo wema wowote nautafakari, nafurahi
Nimehuishwa fikra zangu, nafurahi
Nimeridhika na utauwa kwa bwana
Upendo wa dunia hii una sababu
Sababu hizo zikiisha huisha
Upendo huo ni wa nipe nikupe
Vitu vikienda na upendo umeenda
Furaha ya dunia hii ni ya sababu
Ukivikosa vitu inaisha
Amani ya dunia hii ni ya sababu
Hetengenezwa na mazingira yasiyodumu
Utauwa, na kuridhika vimenipa utoshefu
Utauwa, na kuridhika vimenipa utoshefu
Utauwa, na kuridhika vimenipa utoshefu
Utauwa, na kuridhika vimenipa utoshefu
Nitawapenda watu tena nitawaamini
Ntakupenda zaidi wewe usiyeumiza
Nitafurahi tena nitatabasamu na kuwainyesha mwanya ila sitawapa moyo
Moyo hadanganya
Nitaukabidhi kukupa wewe uliyeuumba, moyo huua
Sitalpa mtu maana haujui
Watu wanatibu ila wewe waponya, wao hunenepesha ila wewe unawandisha
Japo twaanguka twaumia, twateseka tunalia
Wewe bwana ni faraja yetu, nimeridhika
Na utauwa umenipa kutosheka, nimeridhika
Nimekupa moyo wangu utawale
Nimejifunza kuwa radhi, katika hali yeyote niliyonayo
Najua kudhiriwa tena na kufanikiwa katika hali yeyote
Na katika mambo yeyote nimejifunza kushiba na kuona njaa
Nimejifunza kuwa na vingi na kupungukiwa
Nayaweza yote kwa anitiaye nguvu
Nimejifunza kuwa radhi katika hali yeyote niliyonayo
Najua kudhiriwa tena na kufanikiwa katika hali yeyote
Na katika mambo yeyote nimejifunza kushiba na kuona njaa
Nimejifunza kuwa na vingi na kupungukiwa
Nayaweza yote kwa anitiaye nguvu
Watch Video
About Utoshefu
More AMBWENE MWASONGWE Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl