Unikumbuke Lyrics by AMBWENE MWASONGWE


Nimekuita uambie watu ushuhuda wangu
Miaka tisa nimekaa jela
Nilifungwa kwa kosa la kusingiziwa
Namshukuru Mungu nimetoka

Usiku ule nilikamatwa kama mchezo
Na mke wangu na mtoto mdogo
Nikadhani labda walikuwa wanatania
Labda ilikuwa siku ya wajinga

Hakuna mtu alielewa ukweli wa ushahidi wangu
Wala sikuwa na wakumweleza akanielewa
Mazingira ya kesi, ushahidi, sheria za kazi
Siri ni ban, mpaka mke wangu kaniambia
Kama umefanya kiri kosa tujue moja

Nikumbuke, kumbuka haki yangu, sikufanya ubaya
Nikumbuke, nikumbuke, sikufanya ubaya
Nikumbuke, namna walivyonishtaki kwa hila na wivu
Nikumbuke, bwana unikumbuke nililia

Hey, kumbuka bwana haki yangu
Hey, wakumbuke, walivyo kufanikiwa jela
Uwakumbuke, Mungu wakumbuke washa mshumaa ndani ya nyumba
Mkumbuke mtoto mchanga asiye na hatia
Uwakumbuke, kama ningekuwepo angekonda
Kumbuka Adam, aliyebaki, alikufanya kushtuka kwa ajili yako

Nilidhani Mungu kalisahau faili langu
Nikadhani kwamba nitaaibika
Sikuwa tena na tumaini lililobaki
Haki yangu ilikuwa tumaini pekee

Waweza elewa shahidi wangu alikuwa Mungu
Labda na wale walioua
Mwisho wa siku Mungu alinitetea
Na waliofanya kosa kunikana

Haki yangu ikasitana kama mtende na mwelezi
Pale banoni, walinichimba wakuning'oa sababu ya Mungu
Waliinamisha wakunivunja, walinitikisa sikupukutika
Walinichuma ili niishe
Wewe bwana ulinitetea na haki yangu

Nikumbuke, kumbuka maadui walivyonizunguka
Nikumbuke, kumbuka ushahidi wa maneno yao
Nikumbuke, kumbuka walivyonichafua jina langu
Nikumbuke, kumbuka walivyoniona 
Mi ni mhalifu, hey ukalisafishe jina langu

Hey bwana, uwakumbuke! Uwakumbuke Ukarehemu makosa yao
Uwakumbuke! Japo walifanya ubaya bwana na uwasamehe
Uwakumbuke! Nilienda jela nikiwa bado sikujui
Uwakumbuke! Nimetoka nimeokoka nimekujua
Nikumbuke! Bwana unikumbuke usinisahau

Natengeza fadhili zako, niimbe Mungu baba
Nimefurahi, niimbe Mungu bwana
Nimefurahi, niimbe Mungu bwana
Nimefurahi, niimbe Mungu bwana
Nimefurahi, niimbe Mungu bwana

Watch Video

About Unikumbuke

Album : Unikumbuke (Single)
Release Year : 2021
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
Published : Aug 07 , 2021

More AMBWENE MWASONGWE Lyrics

AMBWENE MWASONGWE
AMBWENE MWASONGWE
AMBWENE MWASONGWE
AMBWENE MWASONGWE

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl