Koroga Lyrics
Koroga Lyrics by SAIDAN
Umenifisadi kiuchumi waleti umeiacha zero
Ni wewe wewe mwenye macho ya euro
Ulinidanganya msambaa kumbe mchaga wa Kilimanjaro
Unaipenda pesa kama laini na vocha
Umenifanya ndondocha mi siwazi kukuwacha
Nimedata na penzi maisha majonzi
Mapenzi tulianza juzi unataka nikununulie Benzi
Una mvuto wa ngekewa kujinasua siwezi
Nimesha pata ukweli wewe mi matame
Tanga ulikuja kwa bibi wazazi wako wanaishi Same
Upendo wako kwangu kungu unaashiria jua kali
Na ndoto za utajiri bora kwako ni jazari
Lakini ninafikiri jinsi fulani nitaja nitajihadhari
Nahisi mami umenichanganya akili
Kwa nguvu za tunduli, kitaa wananijadili
Saidan sieleweki, nishageuka ka jokeli
Zila akili za skuli zote utazikabili
Siwazi lile wala hili nakufuata ka kivuli
Eeeh nakufuata ka kivuli, kwenye mvua mi mwavuli
Maana umenikoroga, umenivuruga
Acha tu nikwambie akili umeichanganya wee
Napata dhoruba nimekuwa rubaa
Yaani kwako nang'ang'ana wee
Umenikoroga, umenivuruga
Acha tu nikwambie akili umeichanganya wee
Napata dhoruba nimekuwa rubaa
Yaani kwako nang'ang'ana wee
Maswali mengi nimejiuliza kichwani
Uliporoga ni Handeni ama Pangani
Nakosa jibu nimebaki kuwa bubu
Huu upendo wa dhati naona unanisulubu
Ukiporoga ni kwa bibi ama kwa babu
Dakika tano nikikumisi nalia ajabu
Kwanini kichwani ndo wazo
Na naongea na mtu na unakata mazungumzo
Nimezidi kukupenda mpaka inakuwa tatizo
Ukisafiri nabaki tu stendi
Jua linanichoma mi natekwa na makundi
Upendo gani? Najishangaa
Nyumbani sitoki nilipokaa nimebung'aa
Mapenzi ya dhati hakuna, unanipa kwa mkataba
Sijui ni kipi kilichomfanya nikawa zoba
Umenishawishi nikauza nyumba ya baba
Kwa pressure akafariki sijahudhuria ata msiba
Na ukisema tuachane natamani kujiua
Haki ya Mungu kwa mganga umeniendea
Na uliporoga mpaka sasa sijapajua
Umenikoroga, umenivuruga
Acha tu nikwambie akili umeichanganya wee
Napata dhoruba nimekuwa rubaa
Yaani kwako nang'ang'ana wee
Umenikoroga, umenivuruga
Acha tu nikwambie akili umeichanganya wee
Napata dhoruba nimekuwa rubaa
Yaani kwako nang'ang'ana wee
Umenichoma vibaya, baya
Nasurubika sipati dawa
Umenichoma vibaya, baya
Nasurubika sipati dawa
Watch Video
About Koroga
More SAIDAN Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl