Mwokozi Wetu Lyrics by PAPI CLEVER & DORCAS


Mwokozi wetu anatupa furaha duniani
Atuongoza kwa neema na anatushibisha
Tazama, yupo pamoja nasi, neema haitaisha kamwe
Haleluya, haleluya, haleluya
Amina
Tazama, yupo pamoja nasi, neema haitaisha kamwe
Haleluya, haleluya, haleluya
Amina

Ni vema kumpenda Mungu aliyetukomboa
Vizuri kuwa mtu wake, sitapotea kamwe
Furaha yetu itabakia, ikiwa vyote vingetoweka
Haleluya, haleluya, haleluya
Aminia
Furaha yetu itabakia, ikiwa vyote vingetoweka
Haleluya, haleluya, haleluya
Aminia

Ikiwa giza mara nyingi, na jua likifichwa
Na tukijaribiwa huku twajuwa ni kwa mda
Mbinguni hatutaona kamwe huzuni wala machozi tena
Haleluya, haleluya, haleluya
Aminia
Mbinguni hatutaona kamwe huzuni wala machozi tena
Haleluya, haleluya, haleluya
Aminia

Na tusisumbukie tena chakula wala nyumba
Maana vyote twavipata kwa ne’ma yake Mungu
Njiani yote atuongoza aichukuwa mizingo yetu
Haleluya, haleluya, haleluya
Aminia
Njiani yote atuongoza aichukuwa mizingo yetu
Haleluya, haleluya, haleluya
Aminia

Ikiwa vema huku chini kutegemea Yesu
Furaha gani huko juu kuona uso wake
Tutaiona furaha tele, na utukufu hautaisha
Haleluya, haleluya, haleluya
Aminia
Tutaiona furaha tele, na utukufu hautaisha
Haleluya, haleluya, haleluya
Aminia

Watch Video

About Mwokozi Wetu

Album : Mwokozi Wetu (Single)
Release Year : 2023
Added By : Farida
Published : Jul 12 , 2023

More PAPI CLEVER & DORCAS Lyrics

PAPI CLEVER & DORCAS
PAPI CLEVER & DORCAS

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl