Unataka nini? Lyrics
Unataka nini? Lyrics by MUHONJA
Sitakimbizana na wewe eeh
Sitafuatana na wewe eeh
Sitalia na wewe we
Sitacheka cheka na wewe eeh
Sasa iwaje leo hii
Mwili wangu hutaki tena daddy
Sasa iwaje leo hii
Mwili wangu hutaki tena mpenzi
Eti umepata mwingine
Ni mweupe kunishinda daddy
Eti umepata mwingine
Amebeba kunishinda daddy
Eti umepata mwingine
Amejaza kunishinda daddy yeah yeah yeah
Niambie nitafanya
Nieleze nitatenda
Nijulishe nitambue
Niambie nitafanya
Nieleze nitatenda
Nijulishe nitambue
Wewe unataka nini wewe
Unataka nini?
Unataka nini wewe
Unataka nini?
Niambie nitafanya
Nieleze nitatenda
Nijulishe nitambue
Niambie nitafanya wee
Unataka nini wewe
Unataka nini?
Oooh, oooh ooh...
Aki matusi mateka mangumi
Mume wangu wee mwili unaunama
Majirani, rafiki, watoto
Wazazi wangu wee wamechoka kutatua
Unanijaza huzuni machozi
Mawazo tele kichwa itaruka
Madakitari, machifu, polisi
Wazee wa mtaa, huyu ataniua
Mama, bora nirudi nyumbani
Baba, niruhusu niende
Watanisema watanisimanga
Watanisengenya na bora niko uhai
Watanicheka, watanilaani
Watanitukana, Nina amani
Watanisema watanisimanga
Watanisengenya mimi niko uhai
Watasimanga Wananicheka, watanilaani
Mimi niko uhai
Kama hunitaki tena
Niambie niondoke kuliko kunitesa
Wewe unataka nini wewe
Unataka nini?
Unataka nini wewe
Unataka nini?
Niambie nitafanya
Nionyeshe nitatenda
Nijulishe nitambue
Watch Video
About Unataka nini?
More MUHONJA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl