Itakuwaje (Corona) Lyrics
Itakuwaje (Corona) Lyrics by LINEX
Nashauriwa na wataalamu
Hata mikono yangu mwenyewe
Nisiwe na imani nayo
Kabla ya Corona kuna HIV
Malaria Ebola na mengineyo
Je utamudu maisha kukaa ndani
Tusiende kazini
Au ndo zama za miaka elfu moja
Ya utawala wa shetani
Muulize Mungu wako
Kama kweli ni haki?
Tupunguze kesi za Corona mtaa
Tuanze kuhesabu wangapi
Wanakufa kwa njaa majumbani
Wataishije wasanii bila makongamano
Au waliopo karantini kwa 14 days
Watavichanga watupe show
[Chorus: Mimi Mars]
Nimefunga sali kwa ajili ya dunia
Na taifa lako
Hakuna chenye mwanzo kisicho na mwisho
Pesa haina tena dhamani
Watu wanalilia uhai
[Stamina]
Ah yeah naongea na wewe mr Covid 19, Corona
Mzee wa kuweka watu karantin
Nina familia inayonitegemea mimi
Sasa nikikaa ndani watoto watakula nini?
Mbona Ebola hakututesa kama wewe
Daily tupo na malaria na hatutishi kama wewe
Wewe ni nani mpaka uitese dunia?
Nikiviona vifo vyatajwa ndio kabisa huwa nalia
Hebu nenda na please naomba usirudi tena
Usije tena -- ebu tuwache vyema
Mungu ibariki Tanzania hili nalo litapita
Mungu ibariki dunia
[Chorus: Mimi Mars]
Nimefunga sali kwa ajili ya dunia
Na taifa lako
Hakuna chenye mwanzo kisicho na mwisho
Pesa haina tena dhamani
Watu wanalilia uhai
[Belle 9]
Halina suluhisho hili tatizo
Tusali kwa imani majumbani
Ee Mungu baba tuokoe
Nawaza na wenzangu na mimi
Wale wenye hali za chini
Riziki zao nnje ya mlango
Wafuate mpango, nani atawaletea
[Country Boy]
Hey Corona please I'm talking to you
Unataka nini -- I know what to do
Wtf you came from? umetokea hatuvijui
Kasi haiendi kifupi maisha taabu tu
So we pray to God na hili lipite
Tuwe makini tujilinde ili tusijizike
Watoto wa kiume na kike taarifa zifike
Kaa nyumbani wash your hands alafu msikusanyike
[Chorus: Mimi Mars]
Nimefunga sali kwa ajili ya dunia
Na taifa lako
Hakuna chenye mwanzo kisicho na mwisho
Pesa haina tena dhamani
Watu wanalilia uhai
[Belle 9]
Nawaza na wenzangu na mimi
Wale wenye hali za chini
Riziki zao nnje ya mlango
Wafuate mpango, nani atawaletea
Dunia inasikitika
Machozi yanatutoka
Wagonjwa wanaongezeka
Tiba wapi umefichwa
Dunia inasikitika
[Linex]
Ni kweli Mungu hamtupi mja wake
Lakini kinga ni bora kuliko tiba
Tuyafuate maelekezo
Tunayopewa na wizara ya afya
Tuyafuate maelekezo
Tunayopewa na wizara ya afya
(Itakuwaje?)
[Chorus: Mimi Mars]
Nimefunga sali kwa ajili ya dunia
Na taifa lako
Hakuna chenye mwanzo kisicho na mwisho
Pesa haina tena dhamani
Watu wanalilia uhai
Watch Video
About Itakuwaje (Corona)
More LINEX Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl