Ananiringia Lyrics
Ananiringia Lyrics by LAVA LAVA
(Ayolizer)
Siku hizi hanipigii
Hata akikuta missed call zangu
Simu hashiki na akishika
Anauliza nani mwezangu
Mara anakata
Mara simu hewani haongei
Namaliza vocha
Anajizima data eti amepanda bei
Kunifanya ndodocha
Najitumisha message
Mara mbili mbili
Anafungua anasoma
Majibu hayarudi eh eh eh
Ila kwa Whatsapp page
Zaonyesha tiki mbili
Kujifanya hajaona
Ili mradi kusudi na kunidharau
Ananiringia ringia
Ananiringia ringia
Siku hizi ananiringia ringia
Ananiringia ringia
Anajua nampenda (Basi tu)
Anafanya kusudi kuniumiza (Basi tu)
Ili mradi kuniliza (Basi tu)
Anafanya kusudi kuniumiza (Basi tu)
Ili mradi kuniliza
Aah...aah...aah
[Mbosso]
Na dhalia hainaga suu
Yaliyosemwaga ya kale
Kufurahia kunguru nafuu
Wakigombana mbalale
Moyo unawaka moto kifuu
Yanichoma maumivu mshale
Enyi malaika mlio juu
Shusheni amani itawale
Nayamaliza madhehebu
Kusomewa madua
Mbolea imekausha mbegu
Imeshindwa chipua
Mtazame nampenda kwa sana
Leo unanifanya mi nalia
Ina maana ndo nimechokwama
Au jamaa sina fungu kwenye dunia
Najitumisha message
Mara mbili mbili
Anafungua anasoma
Majibu hayarudi
Ila kwa Whatsapp page
Zaonyesha tiki mbili
Kujifanya hajaona
Ili mradi kusudi na kunidharau
Ananiringia ringia (Ananiringia)
Ananiringia ringia (Ananidengulia)
Siku hizi ananiringia ringia
Anairusha rusha roho yangu
Ananiringia ringia
Anajua nampenda (Basi tu)
Anafanya kusudi kuniumiza (Basi tu)
Ili mradi kuniliza (Ila basi tu)
Anafanya kusudi kuniumiza (Basi tu)
Ili mradi, ila nenda
Nenda mwambie asante
Mwambie asante
Nenda mwambie asante
Mwambie asante
Nenda mwambie asante
Mwambie asante
(Kanifunza maumivu nilikuwa siyajui)
Nenda mwambie asante
Mwambie asante
(Ustahimilivu nisilipize uadui)
(Kwa Mix Lizer)
Watch Video
About Ananiringia
More lyrics from Promise album
More LAVA LAVA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl