SOLOMON MKUBWA Mfalme wa Amani cover image

Paroles de Mfalme wa Amani

Paroles de Mfalme wa Amani Par SOLOMON MKUBWA


Daudi kasema, nilikuwa kijana sasa ni mzee 
Sijawahi kuona mwenye ameachwa mimi 
Wala watoto wake kuombaomba mikate barabarani 
Mungu ni mwaminifu, kwa ahadi zake wanadamu 

Mungu ni mwaminifu, kwa ahadi zake si kama wanadamu
Akiongea Yesu ameongea
Akikuahidia kitu, Baba ameahidi na ujasiri
Atatenda kwa wakati wake 
Ninamwita Bwana wa amani 

Ninamwita mfalme wa amani 
Ndio maana mimi ninaimba kwa sababu ya amani yake 
Ni uwezo gani, uwezo gani unaominga Baba 
Uwezo gani, uwezo gani, uwezo gani
Mfalme wa amani, mfalme wa amani uinuliwe 

Wewe ni mwema, wewe ni mwema Bwana wangu 
Wewe ni mwema, wewe ni mwema Bwana wangu
Wewe ni mwema, wewe ni mwema Bwana wangu

Usilie, usilie, usiliwe wewe 
Usilie Bwana anakujua ndugu yangu 
Amesikia kilio chako wewe mama 
Unalia nini kwa wanadamu, mama yangu

Wanadamu hawatakusaidia na kitu 
Wanadamu hawatakuwezesha kwa kitu chochote 
Tunaye mmoja anayepanguza machozi ya watu wake
Ni yule mfalme wa amani 

Ni yule aliyesema yote imekwisha 
Mama unayoyapitia ni yeye anayeyaona
Anajua shida yako mama yangu 
Anajua magumu yako baba yangu 

Ukiwa na shida usiende kwa waganga wa dunia 
Ukiwa na magumu usiende kwa wafumu wa dunia 
Muite mfalme wa amani, yeye anajibu maombi 
Ni uwezo gani, uwezo gani unaominga Baba 
Uwezo gani, uwezo gani, uwezo gani

Mfalme wa amani, uinuliwe Bwana wangu 
Yale unayotenda inashangaza dunia nzima 
Wanaokosa amani ndani ya nyumba zao wape amani 
Wanaokosa amani ndani ya kazi zao wape amani

Ni wewe Bwana wa amani ya kudumu
Ni wewe Bwana wa amani ya Afrika 
Amerika wanalia amani 
Tunawe Bwana mfalme wa amani 
Hakuna kitu kile kinachokushinda Bwana
Yeye Mfalme wa Amani 

Mfalme wa amani, uinuliwe Bwana wangu 
Yale unayotenda inashangaza dunia nzima 
Wanaokosa amani ndani ya nyumba zao wape amani 
Wanaokosa amani ndani ya kazi zao wape amani

Ecouter

A Propos de "Mfalme wa Amani"

Album : Mfalme wa Amani (Single)
Année de Sortie : 2016
Copyright : (c) 2020
Ajouté par : Huntyr Kelx
Published : Dec 16 , 2020

Plus de Lyrics de SOLOMON MKUBWA

SOLOMON MKUBWA
SOLOMON MKUBWA

Commentaires ( 0 )

Aucun commentaire pour l'instant



A propos de AfrikaLyrics

Afrika Lyrics est la plus large collection de paroles de chansons et de traductions d’Afrique. Afrika Lyrics fournit les paroles des musiques de plus de 30 pays africains et des traductions de lyrics de plus de 10 langues africaines en français et en anglais.

Suivre Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl