Paroles de Ya Dunia
Paroles de Ya Dunia Par SERRO
Hayeye!
Nimesota, sina wera, juzi nilikopa nilipe mama mboga
Hawajui, hawata amini, juu mi ni mwana mziki na mambo yangu iko fiti
Na huko instagrama, wanadhani nimeosa
Sababu waliona nikikula na Obama
Wengi ni mastar kwa vile wanavyo vaa
Lakini utashangaa, vile wanavyokaa
Wengi hujifanya mambo yao yako sawa
Lakini utashangaa, ni mengi haya ya dunia
Hayeye!
Chakula githeri chemsha na avocado
Na nina deni ya soo mbili ya mama Wambo,
Sasa nasaka fare anagalau nifike show.
Lakini jana si nilikua kwa TV, na juzi pia nilikua kwa gazeti,
Mambo yangu yanafaa kua fiti
Huko instagrama, wanadhani niko poa
Sababu waliona, ile poster ya Koroga
Wengi ni mastar kwa vile wanavyo vaa
Lakini utashangaa, vile wanavyokaa
Wengi hujifanya mambo yao yako sawa
Lakini utashangaa, ni mengi haya ya dunia
Sio yote yang’aayo ni dhahabu,
Watu huficha masaibu kwa tabasamu
Basi sote tuwe wakarimu
Sababu yote yang’aayo si dhahabu
Wengi ni mastar kwa vile wanavyo vaa
Lakini utashangaa, vile wanavyokaa
Wengi hujifanya mambo yao yako sawa
Lakini utashangaa, ni mengi haya ya dunia
Ecouter
A Propos de "Ya Dunia"
Plus de Lyrics de SERRO
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Vous aimeriez sûrement
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl