NACHA Nachacetamol cover image

Paroles de Nachacetamol

Paroles de Nachacetamol Par NACHA


Maandishi yangu nayoandika yatakumbukwa hata nikifa
Ntaacha alama, alama ntakumbukwa kama agano jipya
Starehe zitapita, miamba itapasuka
Moyo wangu wa utiifu ukawa mtakatifu peter
Nusu straika, nusu kaswida na dufi
Kichwa kakijatunza moshi zaidi ya msaafu na juzu
Nimezaliwa nyasuri ndo chanzo cha madini haya
Sijazaliwa ufalme wa yupakama nabii isaya
Kabla ya kuhukumu shirikisho na kuweka vitisho
Je? Kuna jitihada zozote za kujikwamua huku tulipo
Ni ngumu kujinagua maana kila mtu ni mpigaji
Kinacho itafuna yanga ni mfumo wa uendeshaji
Demokrasia sio chupa ya bia unaweza kuagiza tu
Inahitaji kulinodwa na kuendelezwa na watu
Hatuwezi kutatua matatizo yetu kina kujifanya hayapo hii ndo inakula kwetu
Yule kahama chama hiki mara yule kawasaliti
Sishangai siasa natamani marafiki
Elimu sio njia ya kuepuka umasikini
Bali hi njia y akupigana na umasikini
Kujifanya tunachofanya hamuoni mnakata stim
Nisawa na kupaka mkongo halafu demu akazima simu
Nilizaliwa kupambana kwahiyo unyonge kwangu katu
Naona mnajichoresha christmass mnapiga daku
Kama  ningepewa fursa wa kuziba palipo bomoka
Ningeanza kujenga maisha ya waalimu na quarter
Tunapojali sekta tusifanye ubaguzi chomde tusiwaache
Nyuma tuma tuwakumbuke wauguzi
Nyasubi mama Farida ndo chatta inapotokea
Afu mchizi ni underated na sio underware
Na siku mkiweka usawa watoto watapagawa
Mitaa ndo iatjua nani adamu nani hawa

Mi naponya maumivu, wananiita nacha getemol
Ukipata maumivu we niite nachaniite nachacetamol
Niite nachacetamol, nachacetamol, nachacetamol
Niite nachacetamol nachacetamol nachacetamol

Hakuna dhambi mbaya ka ya dhuruma sikufichi
Utavishwa sanda maana kita naesi ni mauti
Be humble haina haja ya ukiburi
Maana ghetho la kudumu la mwanadamu ni kaburi
Ombeni nanyi mtapewa
Tafuteni nanyi mtaona
Ubaya ni kwamba tunaamini tunachoona
Midomo dubu mi binafsi inaniboa
Kusubiri viogozi wafe ndo tuanze kuwakosoa
Mama nacha alinambia mkumbo ni ugonliwa zaidi ya ebola
Maana tunaamini aliebora ni yule alieaminiwa na bora
Kuamini kwa kuambiwa itatukosti na itakuboa
Kama kuchepuha halafu ukatia mimba nje ya ndoa
Nacha n genius msipime hizi level
So mtachagua mniite bara ama baba levo
Na nacha ni mmoja hili nasema bila woga
Mbona mnaforce kumlinganisha niyonzima na pogba

Mi naponya maumivu, wananiita nacha getemol
Ukipata maumivu we niite nachaniite nachacetamol
Niite nachacetamol, nachacetamol, nachacetamol
Niite nachacetamol nachacetamol nachacetamol
Nachacetamol, nachacetamol

Ecouter

A Propos de "Nachacetamol"

Album : Nachacetamol (Single)
Année de Sortie : 2020
Ajouté par : Farida
Published : Sep 17 , 2020

Plus de Lyrics de NACHA

Commentaires ( 0 )

Aucun commentaire pour l'instant



A propos de AfrikaLyrics

Afrika Lyrics est la plus large collection de paroles de chansons et de traductions d’Afrique. Afrika Lyrics fournit les paroles des musiques de plus de 30 pays africains et des traductions de lyrics de plus de 10 langues africaines en français et en anglais.

Suivre Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl