Paroles de Nyakati
Paroles de Nyakati Par MARTHA ANTON
Kuna wakati wa kulia
Kuna wakati wa kucheka
Kuna wakati wa furaha
Kuna wakati wa huzuni
Hizo zote ni nyakati
Yakupaza uzipitie
Hizo zote ni nyakati
Yakupaza uzipitie
Kuna wakati wa kuinuliwa we mama wewe
Kuna wakati wa kushushwa chini we mama
Kuna wakati wa kukataliwa na watu wote
Kuna wakati wa kukubaliwa na watu wote
Hizo zote ni nyakati
Yakupaza uzipitie
Usiogope baba we, Mungu yuko nawe
Usiogope mama we, Mungu yuko nawe
Usiogope dada we, Mungu yuko nawe
Usiogope kaka we, Mungu yuko nawe
Jaribu ulo nalo ni la kitambo tu
Tatizo ulo nalo ni la muda tu
Kuna wakati umepitia magumu mengi
Ukasema kwa haya, Mungu hayupo
Kuna wakati umepitia shida nyingi
Ukasema kwa hizi shida, Mungu hayupo
Kuna wakati ulifiwa na mpendwa wako
Ukasema kwa hili, Mungu hayupo
Kuna wakati ulipitia majaribu mengi
Ukasema kwa haya, Mungu hayupo
Umesahau ni nyakati
Yakupaza upitie
Umesahau ni nyakati
Yakupaza uvumilie
Kuna wakati Yesu aliponya wagonjwa wao
Watu wakafurahi wakasema huyu ndiye Mungu
Kuna wakati Yesu aliwapa mikate
Watu wakafurahi na kuchekelea
Kuna wakati Yesu alifanya miujiza mingi
Watu wakafurahi wakasema ni Masihi
Lakini ulipofika wakati wa mateso ya Yesu wangu
Hao hao wakasema asulubiwe eeh
Lakini ulipofika wakati wa mateso ya Yesu wangu
Hao hao wakasema asulubiwe eeh
Hizo zote ni nyakati
Huyu Yesu alipitia
Hizo zote ni nyakati
Huyu Yesu alizishinda
Usiogope baba we, Mungu yuko nawe
Usiogope mama we, Mungu yuko nawe
Usiogope dada we, Mungu yuko nawe
Usiogope kaka we, Mungu yuko nawe
Jaribu ulo nalo ni la kitambo tu
Tatizo ulo nalo ni la muda tu
Usiogope baba we, Mungu yuko nawe
Usiogope mama we, Mungu yuko nawe
Usiogope dada we, Mungu yuko nawe
Usiogope kaka we, Mungu yuko nawe
Jaribu ulo nalo ni la kitambo tu
Tatizo ulo nalo ni la muda tu
Vumilia jipe moyo
Vumilia utashinda ndugu wee
Ecouter
A Propos de "Nyakati"
Plus de Lyrics de MARTHA ANTON
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Vous aimeriez sûrement
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl