Paroles de Corona Ipo Par KALA JEREMIAH


Jihadhari na Corona ipo kila kona
Be aware it is everywhere
Mama, baba eeeh

Jihadhari na Corona
Nawa mikono kila mara usiku na mchana
Epuka misongomano isiyokuwa na maana
Epuka mitoko isiyokuwa ya lazima
Kaa sehemu moja usiwe unaranda randa kila kona

Tufuate maelekezo mamlaka zinasema
Dalili ni mafua na wakati wa kuhema
Kifua kinabana na mwili unapanda homa
Kukohoa kuchoka mwili na kichwa kuuma

Ukisikia hizi dalili wahi kwenda kupima
Watoto kina mama wazee kwa vijana
Nawa mikono kama vile unashindana
Salimiana mbali usidhubutu kushikana

Unakaa mita mbili toka mwingine aliposimama
Kwani hujui kukumbatiana ni noma
Ni noma salamu ziende mpaka kijijini
Mnanawia ndani ya besheni watu ishirini?

Dah wacheni huo utani
Nawieni maji ya kutiririka na sabuni
Tahadhari ni bora kuliko nyama msibani
Epukeni umati siku ya ng'ombe mnadani
Vaa mask ukitaka kwenda mjini ama sokoni
Mwenye maambukizi hana alama ya usoni
So nilinde nikulinde tulindane kama mboni

Jihadhari na Corona ssiku na mchana 
Nah nah nah nah nah
Nawa mara kwa mara kama unashindana
Nah nah nah nah nah

Hili ni janga la kujipanga
Nah nah nah nah nah
Madoctor wanakesha na manesi wanakesha macho
Nah nah nah nah nah

Ongeza sauti maana ya kwanza ilikuwa dibaji
Hakikisha nyumbani una sabuni na una maji
Corona isilete mimba za utotoni na ubakaji
Shule hazikufungwa ili ngariba akuze mtaji

Ona tiyari kuna kesi za ukeketaji
Wazazi mbona tena watoto mnahujumu
Ndoa za utotoni ni ukatili na hazidumu
Baba mama walezi na ndugu mna jukumu

Kuhakikishia watoto amani nyumbani inadumu
Kwenye ndoa chunga Corona isije igeuke sumu
Baba unampiga mami ati kisa kashika simu
Kisha kakuuliza kuhusu message ya Mwantumu

Hofu na msongo wa mawazo hebu tupa kule
Wape watoto uhuru nyumba waigeuze shule
Hakikisha wanashinda ndani wasizurure
Shule zimefungwa ili kukwepa msongomano (Right?)

Sasa mbona wanazurura mpaka night?
Mama zetu ndio mahero tunajua
Mnapambana sana mpaka sisi tunakua
Sasa nawakumbusha tahadhari kuchukua

Unapokohoa ziba kwa kiwiko mdomo na pua
Nawa mikono tena mbele na nyuma sugua
Jihadhari na Corona maana ipo na inaua
Usijiguze usoni ni marufuku mmenisikia?

Jihadhari na Corona ssiku na mchana 
Nah nah nah nah nah
Nawa mara kwa mara kama unashindana
Nah nah nah nah nah

Hili ni janga la kujipanga
Nah nah nah nah nah
Madoctor wanakesha na manesi wanakesha macho
Nah nah nah nah nah

Tuko vitani, na kila mmoja wetu ni askari
Kila mmoja wetu anatakiwa kuchukua hatua
Za madhubuti za kujidhibiti adui Corona
Adui yuko kwenye kona

Sababu tunazo, uwezo tunao
Nguvu tunazo za kupiga adui Corona
Kwa kunawa mikono kila wakati
Kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima

Hakikisha kila ukitoka umevaa barakoa au
Maski kwa jina jingine

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Africa
Mungu ibariki dunia 
Mungu wabariki wauguzi

Nesi na madaktari 
Na watu wote wanaohusika
TUTASHINDA!

Ecouter

A Propos de "Corona Ipo"

Album : Corona Ipo (Single)
Année de Sortie : 2020
Copyright : (c) 2020
Ajouté par : Huntyr Kelx
Published : May 06 , 2020

Plus de Lyrics de KALA JEREMIAH

KALA JEREMIAH
KALA JEREMIAH
KALA JEREMIAH
KALA JEREMIAH

Commentaires ( 0 )

Aucun commentaire pour l'instant



A propos de AfrikaLyrics

Afrika Lyrics est la plus large collection de paroles de chansons et de traductions d’Afrique. Afrika Lyrics fournit les paroles des musiques de plus de 30 pays africains et des traductions de lyrics de plus de 10 langues africaines en français et en anglais.

Suivre Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl