Paroles de Haki Za Watoto
Paroles de Haki Za Watoto Par JUALA SUPERBOY
Haki za watoto zitimizwe
Wanalia, wanadhulumiwa
Watoto wanalia
Tusiwatese watoto tuwajenge
Na tuwashughulikie mtaani
Ya zamani yashapita tuangalie
Amani kote kwa watoto tusiwatumie
Tuwapende tuwahisi, ajali tuwajalie
Kwa shari tusiwatupe na pia kuwapuuza
Na wala kuwatusi tukisema hao ni looser
Kumbuka hao tu ni viongozi tu wa kesho
Wakilia wapanguze tu machozi kwa leso
Wanalia, wanadhulumiwa
Watoto wanalia
Wanalia, wanadhulumiwa
Watoto wanalia
Tushikane tuwasaidie
Watoto wapate haki zao
Tushikane tuwasaidie
Tushikane tuwasaidie
Watoto wapate haki zao
Tushikane tuwasaidie
(Eeh eh eh eh eh)
Tazama watoto wetu wanazama huku kwa dunia
Wengine wanacheka kuwaona kwenye njia
-- mpaka mabaya kuwafanyia
Ukimwi unawapata na magonjwa mengine pia
Watoto kuajiriwa kazi ngumu kufanyia
Wengine kutumiwa kwenye wizi hata pia
Hawaoni ni hatari shule kuwaharibia
Mambo haya si mazuri ni mabaya narudia
Waafrika tushikane tuweze kuwasaidia
Watoto hawa wetu wasije kuangamia
Mambo mengi wajifunze ya elimu na dunia
Tuanze kuwapenda wawe wakifurahia
Wanalia, wanadhulumiwa
Watoto wanalia
Wanalia, wanadhulumiwa
Watoto wanalia
Tushikane tuwasaidie
Watoto wapate haki zao
Tushikane tuwasaidie
Tushikane tuwasaidie
Watoto wapate haki zao
Tushikane tuwasaidie
(Eeh eh eh eh eh)
Malezi(Wapate)
Elimu(Wapate)
Afya bora(Wapate, wapate)
Kwa kucheza(Wapate)
Na ulinzi(Wapate)
Na upendo(Wapate, wapate)
Tushikane tuwasaidie
Watoto wapate haki zao
Tushikane tuwasaidie
Tushikane tuwasaidie
Watoto wapate haki zao
Tushikane tuwasaidie
(Eeh eh eh eh eh)
Ecouter
A Propos de "Haki Za Watoto"
Plus de Lyrics de JUALA SUPERBOY
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Vous aimeriez sûrement
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl