ECHO Wapi Uliko cover image

Wapi Uliko Lyrics

Wapi Uliko Lyrics by ECHO


Natumai barua yangu
Umeipata mwandani wangu
Majanga uloyaacha kwangu
Umeupa majeraha moyo wangu

Tangu uondoke naikeshea pombe
Najiona tope yaani songa mazonge
MMmh hata bora ungeniambia
Kama utachelewa kuliko ulivyonisusia

Chakula nimekisusia
Pombe naifanya dinner
Hivi kweli na ulikimbia
Umenisababisha nalia

Umewapa nafasi wanaongea
Kutwa nashinda kudoea
Umewapa nafasi wanaongea
Kutwa nashinda kudoea

Wapi uliko? Nimekutafuta sana mama
Wapi uliko? Kuja uyaponze majeraha
Wapi uliko? Majirani wananisemezana
Wapi uliko?  aah

Acha nijiradhi niongee nawe
Nishalia nusu nipagawe
Majeraha huu ni moyo dada sio mawe
Na ningejua singekubali kuwa nawe

Wapi uliko niambie ni nani alikugeuza mchipuko
Kwa mashangazi na mjomba haupo
Basi ungeniaga kwa rafiki zako

Sioni faida ya mapenzi ikiwa umeniacha mazima
Najihisi kama mkiwa malenganisho yatima
Nimekutafuta kila kona kila kina 
Sijakuona na hata simu yako ulizima

Nikisema tumeachana nitawapa sababu gani?
Wewe hujui tu umekuwa ngumzo kwa majirani
Chizi haswa limenipanda ruhani
Mbona uninyime silaha alafu uniingize vitani

Ishazimaga kibatari, penzi umeniachaga vitani
Mpenzi umeniachaga vitani
Naadhirika hadharani, Wakunipenda tena nani?

Mwenzako nina moyo sina jiwe
Eeh kifaa lawama kwako wee
Yaani umenipiga changa la moto
Kibeli nimeshalala nacho iyee

Chakula nimekisusia
Pombe naifanya dinner
Hivi kweli na ulikimbia
Umenisababisha nalia

Umewapa nafasi wanaongea
Kutwa nashinda kudoea
Umewapa nafasi wanaongea
Kutwa nashinda kudoea

Wapi uliko? Nimekutafuta sana mama
Wapi uliko? Kuja uyaponze majeraha
Wapi uliko? Majirani wananisemezana
Wapi uliko?  aah

 

Watch Video


About Wapi Uliko

Album : Wapi Uliko (Single)
Release Year : 2021
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jul 06 , 2021

More ECHO Lyrics

ECHO
ECHO
ECHO

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2022, We Tell Africa Group Sarl