Watakuheshimu Lyrics
Watakuheshimu Lyrics by ANISET BUTATI
Mpe simu yangu Butati
Pengine kuna kitu ataongea
Natafuta faraja ya moyo wangu
Maumivu makali yananitese
Natafuta faraja ya moyo wangu
Dharau zimezidi naumia
Sababu ya umaskini nadharauliwa
Mchumba wangu kapewa rafiki yangu
Aliyesema umasikini haufai
Namuunga mkono yamenitokea
Nateseka moyo wangu kwa dharau
Ndio maana napiga simu Kigoma
Natafuta faraja kwa mtumishi wa Mungu
Butati kuna nini utaongea juu yangu
Kuna kipindi unapita
Hata watu wakikutazama
Wanakuona
Kutoinuka tena
Kuna kipindi unapita
Hata ndugu wakikutazama
Wanakudharau
Wanajua ni mwisho wako
Wameinuka wamesema
Ati mkufuru Mungu ufe
Mungu gani?
Mbona hakusaidiii
Wameinuka wamesema
Ati mkufuru Mungu ufe
Mungu gani?
Mbona hakusaidiii
Leo waambie, waambie
Nina Mungu ataniinua
Mtaniheshimu
Leo waeleze, waeleze
Nina Mungu ataniinua
Mtaniheshimu
Wewe usimuache Mungu
Wewe mtazame Mungu
Wewe usimuache Mungu
Wewe mtazame Mungu
Wakati wako ukifika wewe
Wa kuinuliwa na Mungu
Waliokuona huna dhamani
Watakuheshimu tu
Wakati wako ukifika wewe
Wa kuinuliwa na Mungu
Waliosema hutoinuka
Watakuheshimu tu
Wakati wako ukifika wewe
Wa kuinuliwa na Mungu
Waliosema ni mwisho wako
Watakuheshimu tu
Wakati wako ukifika wewe
Wa kuinuliwa na Mungu
Waliosema hutofanikiwa
Watakuheshimu tu
Acha leo wakuone wanavyokuonaga
Wakati wa Mungu utaongea
Acha leo wakuite majina mabaya mabaya
Wakati wa Mungu utaongea
Wanaokuita mlala hoi, watazame nyamaza
Hao ndio watakuita bosi kesho
Wanaokuita fukara, watazame nyamaza
Hao ndio watakupigia magoti kesho
Hata Yusufu alikuwa house boy
Wakati wa Mungu alikuwa waziri mkuu
Wewe usimuache Mungu
Wewe mtazame Mungu
Wewe usimuache Mungu
Wewe mtazame Mungu
Wakati wako ukifika wewe
Wa kuinuliwa na Mungu
Waliokuona huna dhamani
Watakuheshimu tu
Wakati wako ukifika wewe
Wa kuinuliwa na Mungu
Waliosema hutoinuka
Watakuheshimu tu
Wakati wako ukifika wewe
Wa kuinuliwa na Mungu
Waliosema ni mwisho wako
Watakuheshimu tu
Wakati wako ukifika wewe
Wa kuinuliwa na Mungu
Waliosema hutofanikiwa
Watakuheshimu tu
Watch Video
About Watakuheshimu
More ANISET BUTATI Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl