RAPCHA Fungua  cover image

Fungua Lyrics

Fungua Lyrics by RAPCHA


Fungua
Oya mwanangu vipi?
99 mwanangu
Mbona kinyonge?
Ahhh
Ndo shida hiyo ya kubetia team msizozijua hahah
Ahh sio kubet
Najua babu
Ila umekaa kimya kinoma nini shida mwanangu
We acha tu mwanangu si unamuelewa huyu shemeji yako
Jinsi ambavyo nna mkubali
Aah naelewa
Halafu kuna miyeyusho flani anakua ananiletea ambayo sio
Yani kama hivi kuna story ambazo mi nakua nazisikia
Lakini nikitaka kumwambia yani koo langu linakua kama
Kuna kitu kimenishikilia hapa nashindwa kuongea yani
Kwasababu najua nikimgusa tu hivi kidogo anakasirika anakuja juu
Ila nataka kinoma kumchana sa sjui tu naanzia wapi mwanangu
Aaah Kwahiyo tatizo ndio hilo
Ndio hivyo mwanangu
Chukua kwanza kitu hichi
Au sio
Piga mbili ukimaliza hicho mwanangu utakua na nguvu
Ya kumchana mbona suala dogo Kula kitu maliza mchane

Uhakika??
Imeisha hiyo baba
Mmmh naam naam
Uuuu chapa chapa chapa yeah yeah ye ye yeee
Mambo mengine mambo madogo mwanangu anakua anawaza
Cough
Mwanangu hiki kama chenye
Msumbiji hiyo baba
Sasa mwanangu
Oi oi oi
Ngoja mi nicheze (mara moja hii umemaliza kitu??)
Nikamkute huko huko aliko kwake nikamuanzishie kama vipi
Aina noma simu zilie mzee simu zilie babaaa
Hizi kengele huyu anahisi nacheza nini?

Fungua inamaana huskii hii kengele au utaka nije tu kukulabua
Kama mnafichana ndani ya makabati leo nitawasha moto hii nyumba ndo mtanitambua
Skia em fungua usitake nijaze watu waje waokote tu vipande maana watakuta nishakupasua Sasa basi napiga kengele mara ya mwisho na navunja kama hutaki kufungua
Oya em Fungua ushaniweka zaidi ya nusu saa nakubishia hodi hutaki kufungua

Ila Hawa kenge wanaokufata sehemu nayolipa kodi wakigonga mlango na miguu unafungua
Sasa Kabla sijapita na huu mlango mpaka ndani na kutibu jeuri yako nitapokubutua
Ngoja nahesabu moja mpaka tatu nauvunja maana nishagonga sana hadi vidole vimeungua
Majirani wananambia kuna njemba napishana nazo sana zinaingia mi nikiwa sipo
Na ndio maana unanambia nikitaka kuja niwe nakupigia leo nimetimba bila info
Hivi kitu gani nitakupa we mwanamke ukatulia
Ukatuliza na roho yangu ikatulia
Nshakuambia mara ngapi hujasikia
Na nazidi kurudia sasa leo utajutia nakuapia
Juzi juzi niliona tu umeshare snapchat uko level one na pembeni
Yako kuna mchizi Nikadaka boda nikufate nafika sijakuona
Nikaambiwa kuwa ushasepa the deez Najitahidi nisikuchunguze
Ila story zinanifikia na kiukweli zinanipa uchizi
Picha zako zote ndani ya gari tofauti unabadili tu mikao huku unachezea keys
Kuleta rafiki zako wa kiume kwenye nyumba niliyokupangia
Kwanza nshakupiga marufuku Wanajiachia sebleni na vipensi
Wanacheza na rimoti kama wanachangia luku
Na hawatosheki na chakula unachowapikia maana wanakula mpaka yule anaewapikia Navyogaramia na mateso unayonipatia hii nyumba mara mia nifugie kuku (kwenda)
Staki hizi mbichi ooh naah
Ukakasi mwingi staki staki staki hili bichi ooh naah
Kukupenda staki hii ni homa

Nimekoma tena staki staki hii sonona, noma
Kuna namba umeisave Daddy kwenye simu yako
Nimeshtuka hata kumbe huyo sio babaako
Unajifanya huna makuu bonge la pretender
Kuna story nimeskia sikuhizi we ni blender
Fungua, kabla sijasema vyote fasta fasta
Fungua, lazima nitapata kesi navunja kitasa
Fungua, staki ufala leo utapata unachokitaka
Fungua, mapenzi nikache staki, bomboclat
Kabla sijakuacha nitakufunza adabu bwana utaempata huko atakuta
Umeshashika adabu Hizi tabu juu ya tabu nimeshindwa ustaarabu
Kama Ndoa nishatoa kwenye hesabu ushanikata vibe

Watch Video

About Fungua

Album : To The Top Vol 2 (Album)
Release Year : 2023
Added By : Farida
Published : Jul 18 , 2023

More RAPCHA Lyrics

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl