NAOMI MUTHEU Wa Kupewa Sifa cover image

Wa Kupewa Sifa Lyrics

Wa Kupewa Sifa Lyrics by NAOMI MUTHEU


Wa kupewa sifa ni wewe Bwana
Na utukufu wote ni wewe Bwana
Wa kupewa sifa ni wewe Bwana
Na utukufu wote ni wewe Bwana

Maana wewe wazistahili zote
Maana wewe peke yako ni Mungu
Maana wewe wazistahili zote
Maana wewe peke yako ni Mungu

Utukuzwe

Juu mbinguni hakuna wa kufa'na nawe
Humu duniani hakuna mfano wako
Chini ya nchi hakuna kabisa
U juu ya yote, u wa pekee
Una mamlaka yote Bwana
Hakuna Mungu kando yako Yahweh

Unayetuokoa a Bwana
Unayetutegemeza twakusifu
Watutia nguvu za kuendelea
Tunapochoka watuhimarisha
Kwa rehema na neema zako Mwokozi
Hakuna kama Wewe 
Hakuna kama We
Hakuna kama wewe e Yahweh eee

(U wa neema Yesu na mwingi wa rehema)

U wa neema Yesu na mwingi wa rehema
Kwa neema yako Messiah umetuleta hapa
Katufilia msalabani tupate wokovu
Tunayashinda majaribu kwa neema yako

Wengine tulisahaulika 'katumbuka Baba
Toka mavumbini 'katuketisha na wafalme
Umetufanya ufalme na makuhani wako
Tunakuinua leo Yesu u wa neema

Watch Video


About Wa Kupewa Sifa

Album : Wa Kupewa Sifa (Single)
Release Year : 2020
Copyright : (c) 2021
Added By : Naomi Mutheu
Published : Jan 07 , 2021

More NAOMI MUTHEU Lyrics

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2023, We Tell Africa Group Sarl