Kwaheri Corona Lyrics
Kwaheri Corona Lyrics by MRISHO MPOTO
Corona funga virago utuwache salama
Sisi ni wamoja vita tutaishinda pamoja
Tanzania, twailinda Tanzania
Dunia, tupambane kwa pamoja
Tanzania, twailinda Tanzania
Dunia, tupambane kwa pamoja
Corona wewe ni nani?
Umekuja kwa ajili ya nani?
Unahitaji nini tukupe uondoke
Tuko tayari kukuchinjia jogoo
Tuliyemweka kwa ajili ya mbegu
Lakini kabla ya kumla jogoo wetu
Tukujulishe sisi ni kina nani, ukoo wa nani
Ili tusije kulaumiana siku za usoni
Corona sisi ni Tanzania, wajukuu wa Nyerere
Tunayeongozwa na jemedari wetu Magufuli
Timu ya ushindi
Kuna makabila mia moja na ishirini
Watu milioni hamsini na nane
Kumbuka Corona wewe ni Kidudu tena mmoja
Sisi ni wamoja, wenye uzalendo, utaifa ndani yetu
Linapokuja janga kama la ujio wako
Tunakuwa kitu kimoja tunaungana
Je tukuchinjie jogoo wetu au utaondoka?
Corona funga virago utuwache salama
Sisi ni wamoja vita tutaishinda pamoja
Tanzania, twailinda Tanzania
Dunia, tupambane kwa pamoja
Tanzania, twailinda Tanzania
Dunia, tupambane kwa pamoja
Corona baada ya uhuru
Mwalimu alitangazia umma maadui watatu
Ujinga, maradhi na umasikini
You know what? Tulimtandika asubuhi na mapema
Maana sababu na utayari tulikuwa nao
Corona umesimamisha dunia sio kama hatuoni
Eti umekuja kwa matone ya mdomoni na puani
Unaingia kwa kushikana mikono, hahahaha
Corona watu hawalali wanakuwaza wewe tu
Nataka niwakute kwa wingi haya, tumegoma kukusanyika
Nitawapata kwenye salamu za mikononi, hatushikani mikono
Kwenye mahaba na mapenzi je? Corona, corona angalia ooh
Kumbuka maji na sabuni tunazo
Na hatua tano za kunawa tunazijua
Tumeshawaelekeza watoto wetu, wajukuu zetu
Vilembwe vining'ina vyote nchi nzima
Yakwamba unaponawa, lowanisha mikono yako
Paka sabuni sugua kona zote
Suuza mikono yako kwa maji tiririka
Jifute kwa kitambaa safi au kung'uta
Corona tunakueleza haya
Ili uondoke kwa hiari yako mwenyewe
Ndugu zangu wa Tanzania ili kushinda vita hii
Kila mmoja wetu ana nafasi ya kunawa mikono
Kulinda nchi yetu ya Tanzania
Corona funga virago utuwache salama
Sisi ni wamoja vita tutaishinda pamoja
Tanzania, twailinda Tanzania
Dunia, tupambane kwa pamoja
Tanzania, twailinda Tanzania
Dunia, tupambane kwa pamoja
Watch Video
About Kwaheri Corona
More MRISHO MPOTO Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl