Nidhibiti Lyrics
Nidhibiti Lyrics by JUX
Una hali gani unayefanya moyo wangu unadadarika
Niko twabani umeniacha dakika mbili tu nishaboreka
Umeniweka rehani
Changu kiwiliwili moyo umeuteka
Umeniathiri honey nshaaribika mbaya kwa yako makopa
Kama mapenzi kitabu
Ungekuwa kurasa ya katikati
Ukichanwa wewe stori haiendelei
Aah aah nakupenda mpaka adhabu baby nahisi kuna hatihati
Ukiniacha wewe walahi mimi sitoboi
Honey honey (Honey) Wangu wa ubani bani
Mimi ndege wako sa manati ya nini
Nakupa ruhusa wee
Nidhibiti Nidhibiti Nidhibiti
Nakupa ruksa wee
Nidhibiti Nidhibiti Nidhibiti
Ewee baby (Ewee baby)
Mke wangu (mume wangu)
Mimi na wee hadi milele
Ooh mbivu ziwe mbichi ni vya kwetu sisi
Sijali nisharidhia yayaah
Wabaya wanafiki watafute viti wakae kwa kutulia hayaa
Upendo kwetu faradhi umepita tsunaa
Rabiii atuhifadhi mpaka kufika chanaa
Ooh na mimi kwako ni radhi kufa kuzikanaaa
Waambie wavunje nazi si tumeshindakana
Honey honey (Honey)
Wangu wa ubani bani
Mimi ndege wako sa manati ya nini
Nakupa ruhusa wee
Nidhibiti Nidhibiti Nidhibiti
Nakupa ruksa wee
Nidhibiti Nidhibiti Nidhibiti
Watch Video
About Nidhibiti
More JUX Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl