ISHA MASHAUZI Sudi Sudini  cover image

Sudi Sudini Lyrics

Sudi Sudini Lyrics by ISHA MASHAUZI


Mja hapati, hapati alitakalo
Bali hupata, ajaliwalo na Mungu
Usikonde, kwa hili nilipatalo
Hilo ndilo, hilo ndilo langu fuu

Mja hapati, hapati alitakalo
Bali hupata, ajaliwalo na Mungu
Usikonde, kwa hili nilipatalo
Hilo ndilo, hilo ndilo langu fuu

Sudi, sudi sudini
Bahati ya mwenzio, usilale mlango wazi
Sudi, sudi sudini
Bahati ya mwenzio, usilale mlango wazi

Ni lipi nililowakosea?
Mbona yenyu ni machafu hamsemi
Mabaya, kutwa kunipakazia
Kama nina deni niambieni

Maana kila siku maneno
Mie si mtu, hilo linatoka wapi?
Mmenibadilisha jina naitwa mchawi
Tena hasidi, yote yanatoka wapi

Maana kila siku maneno
Mie si mtu, hilo linatoka wapi?
Mmenibadilisha jina naitwa mchawi
Tena hasidi, yote yanatoka wapi?

Niliyajua mapema ndo maana nikapuuzia
Washa zoea kusengenya ndo maana nawapotezeaga
Si hofii mi wenu unafiki, shingoni sijitii kamba
Wajidanganya na vyenyu visiki, sumu yenyu sitoilamba
Alopewa na Mola hapokonyeki, wala msijisumbuke kwa dumba 
Wajidanganya na vyenyu visiki, sumu yenyu sitoilamba

Mwanitangazia, mwajitangaza mitaani
Kwamba mnanijua, mimi kiundani wewe
Kuliko hata alonileta duniani wewe

Tena mnajinadi, huko mitaani wewe
Kwamba mnanijua, mimi kiundani wewe
Kuliko hata alonileta duniani wewe

Nyie kama mahodari basi naye mseme
Yaani nyie kibindoni wana wa wezenu midomoni
Nyie kama mahodari basi naye mseme
Yaani nyie kibindoni wana wa wezenu midomoni

Sudi sudini, asiye bahati habahatishi
Sudi nichukie nyinyi, tamaa hamnikatishi
Mwajipatia dhambi nyinyi, nalala mie sikeshi

Ikiwa kuna kuozwa nahisi nimetenda
Basi niko radhi chini niweke mimi
Kuliko kukaa pembeni, mabaya kuzua
Na mimi nina roho, kama nyinyi

Hata ukiwa mwerevu wao watakugeuza ng'ombe
Kusudi wakupake majivu, hao hawana aibu viumbe
Nafeli kwa kukosa usikivu, hamna subira hata chembe
Mnapoteza mwenzenu kwa mambo yenu ya kizembee

Sibabaiki na yenu majungu mie
Mie nawaua kisugu mie
Mwasaka kiti kupitia jina langu
Ukimya ndo sina haya hangu mie
Mmesahau kuwa kuna Mungu
Mwapinga ramli chini ya uvungu nyie

Sudi sudini, asiye bahati habahatishi
Sudi nichukie nyinyi, tamaa hamnikatishi
Mwajipatia dhambi nyinyi, nalala mie sikeshi

Sudi sudini, asiye bahati habahatishi
Sudi nichukie nyinyi, tamaa hamnikatishi
Mwajipatia dhambi bure, nalala mie sikeshi

Pole, pole sana eeh
Pole, pole sana eeh
Na kila kitu mimi
Mimi mchawi wako mimi
Mimi hasidi yako mimi
Mimi na ubaya wako mimi 
Kila kitu mimi

Pole, pole sana eeh
Pole, pole sana eeh
Umeshinda ugangani, kesha uchawini
Sina hirizi shingoni, shina ushale mwilini
Mimi najiamini, namtegemea maanani

Pole, pole sana eeh
Pole, pole sana eeh
Na kila kitu mimi
Mimi mchawi wako mimi
Mimi hasidi yako mimi
Mimi na ubaya wako mimi 
Kila kitu mimi

Pole, pole sana eeh
Pole, pole sana eeh

Kuna nazi, kuna nazi
Kuna nazi, haya kuna nazi
Kukuna nazi kwahitaji ujuzi wewe
Kama hujui nenda muulize somo yako
Kukuna nazi kwahitaji ujuzi wewe
Kama hujui kamuulize somo yako wee

Mi mwenzangu anakuna nazi, haya kuna nazi
Haya imba mwenzangu anakuna nazi, haya kuna nazi
Nazi kweli jamani inampendwa wewe
Ila kukuna eeh yahitaji ujuzi wee
Na iwapo wataka kujaribu wewe
Basi nenda uulize wenye ujuzi wee
Angalia usilete upuzi wewe
Kukuna nazi kwahitaji ujuzi wee

Mi mwenzangu ana-kuna nazi, haya kuna nazi
Haya sasa mimi na kuna nazi, haya kuna nazi

Kukuna nazi kwahitaji ujuzi wewe
Kama hujui nenda muulize somo yako wee
Mi mwenzangu ana-kuna nazi, haya kuna nazi
Mi hodari kukuna ee kuna nazi, haya kuna nazi
Haya imba mwenzangu ana-kuna nazi, haya kuna nazi

Sitaki, sipendi, naogopa
Anajijua yeye kwamba yeye si mzima
Anataka kumpa mwenzake maradhi
Anajijua yeye kwamba yeye si mzima
Anataka kumpa mwenzake maradhi
Kwa makusudi

Sitaki, sipendi, naogopa, sitaki
Anajijua yeye kwamba yeye si mzima
Anataka kumpa mwenzake maradhi
Anajijua yeye kwamba yeye si mzima
Anataka kumpa mwenzake maradhi
Kwa makusudi

Sitaki, sipendi, naogopa, sitaki

Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo
Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo
Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo

Maneno ya watu wanapenda uwongo(Hicho kiranga)
Ua fisi wapi ? Kutwa kimbelembele(Hicho kiranga)
Watu washamjua pembeni wanamcheka oooh

Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo
Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo

Ugomvi si wake kutwa kimbelembele(Hicho kiranga)
Kuchukia watoto wa wenzake bila sababu(Hicho kiranga)
Kuingililia maneno yasiyo mhusu(Hicho kiranga)
Wenzake washamjua pembeni wanamcheka 

Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo
Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo
Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo

Chachizi ukimpa tatizi alitatue ni tatizi(Haha)

Watch Video

About Sudi Sudini

Album : Sudi Sudini (Single)
Release Year : 2018
Copyright : (c) 2018
Added By : Huntyr Kelx
Published : Sep 05 , 2019

More ISHA MASHAUZI Lyrics

ISHA MASHAUZI
ISHA MASHAUZI

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl