NEEMA GOSPEL CHOIR Unirehemu cover image

Paroles de Unirehemu

Paroles de Unirehemu Par NEEMA GOSPEL CHOIR


Unirehemu Mungu unirehemu
Mimi Bwana mungu wangu naja
Maana nafsi yangu imekukimbilia wewe Bwana
Nafsi yangu ikatikati ya Simba
Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale
Na ndimi zao ni upanga mkali peke yangu mimi siwezi
Wameweka wavu iii kuninasa
Nafsi yangu imeinama
Wamechimba shimo mbele yangu, wametumbukia ndani yake
(Bwana uniumbie moyo safiiii ni-kutumikie)
Bwana uniumbie moyo safi
Ili ni-kutumikie
Bwana uniumbie moyo safi
Ili ni-kutumikie
Bwana uniumbie moyo safi
Ili ni-kutumikie

Nimekukimbilia wewe Bwana wangu
Ili nisiahibike milele, kwa haki yako uniponye uniokoe
Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu
Uwe kwangu baba yangu, niumbie moyo safi
Nakuhitaji
Bwana Yesu maishani mwangu
Niumbie moyo safi, Ili nitembee katika kweli yako
Hii ndo haja ya moyo wangu Bwana unisikie
Niumbie moyo safi, niko mbele zako Bwana ninakuomba
Bwana uniumbie Moyo safi
Bwana uniumbie moyo safi
Ili nikutumikie
Bwana uniumbie moyo safi
Ili nikutumikie

Walinizunguka, naam walinizunguka, watesi wangu
Lakini kwa jina la Yesu, naliwakatilia mbali
Walinizunguka, naam walinizunguka, watesi wangu
Lakini kwa jina la Yesu, naliwakatilia mbali
Yesu wewe unaweza
Yesu wewe unatosha
Watumishi wako wote
Utawalinda na kuwatunza
Yesu wewe unaweza
Yesu wewe unatosha
Watumishi wako wote
Utawalinda na kuwatunza
Walinizunguka, naam walinizunguka, watesi wangu
Lakini kwa jina la Yesu, naliwakatilia mbali
Walinizunguka, naam walinizunguka, watesi wangu
Lakini kwa jina la Yesu, naliwakatilia mbali
Yesu wewe unaweza
Yesu wewe unatosha
Watumishi wako wote
Utawalinda na kuwatunza
Yesu wewe unaweza
Yesu wewe unatosha
Watumishi wako wote
Utawalinda na kuwatunza

Ecouter

A Propos de "Unirehemu"

Album : The Sound of Ahsante (Album)
Année de Sortie : 2022
Ajouté par : Farida
Published : Apr 20 , 2022

Plus de Lyrics de NEEMA GOSPEL CHOIR

NEEMA GOSPEL CHOIR
NEEMA GOSPEL CHOIR
NEEMA GOSPEL CHOIR
NEEMA GOSPEL CHOIR

Commentaires ( 0 )

Aucun commentaire pour l'instant



A propos de AfrikaLyrics

Afrika Lyrics est la plus large collection de paroles de chansons et de traductions d’Afrique. Afrika Lyrics fournit les paroles des musiques de plus de 30 pays africains et des traductions de lyrics de plus de 10 langues africaines en français et en anglais.

Suivre Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl