Paroles de Grow Up
Paroles de Grow Up Par NACHA
(Kiri)
Ladies and Gentlemen
I go by the name N.A.C.H.A aka Nacha
Mnyasubi ndani ya mbanyu beiby
Asante Mungu kwa kunipa pumzi ambayo silipii ushuru
Nisipokushukuru ni dhahiri moja kwa moja nakukufuru
Asante kwa kunipa nafasi ya kuongea na wanao nisikiliza
Ili nijue kama wameshakuwa au wanahitaji
Kumwagiliziwa mbolea ili kukua
Tunahitaji kugrow up maana tuna akili finyu kwa kuwa
Tunaweza kulipia hoteli elfu hamsini
Kufanya sex alafu condom ni ya mia tano tu
Ikatushinda kununua, nobody care
GROW UP!
Ajira zimekuwa ngumu
Kaka yangu kahitimu chuo kikuu cha Dar es Salaam
Kaamua kujikita kwenye michezo ya kubahatisha
Swali ni je? Kubet ndio kitu alisomea
Kutoka Standard One mpaka chuo?
GROW UP aisee wavalisheni nguo
Mi huwanga sichukuliangi vitu personal though
Kuna mtangazaji aliyesema kumpa Nacha interview
Ni mpaka awe na demand mtaani
Question hiyo demand nitaipata vipi
Wakati nahitaji kusupportiwa ili niwe na hiyo demand mtaani
Yaani ni sawa na mtu kutoka chuo na kuomba kazi
Alafu unamwambia ni lazima awe na uzoefu wa hiyo kazi
Nonsense!
Sababu za kiintelejesia
Utapasuka msamba ukijaribu kuwaiga
Na ukijaribu tu kuupaza tu sauti na kuwauliza
Kwa nini nyinyi mnakula vya juu?
Watakujibu tunakula vya juu
Kwa sababu tuna shingo za twiga(Mschew)
Huo ni ubinafsi ulafi na uchoyo
Wa kutaka wao pekee yao
Na ndugu zao mikono yao iende kinywani
Alafu mikono yako iende shavuni
Take care GROW UP!
Bado nawashangaa wadau wa kandanda Bongo
Kukiponda chama cha mpira cha nchi hii kiko ovyo
Eti tu kisa National team haijafuzu World Cup ama AFCON
Nina swali nataka majibu sio kingine
Serikali inasupport soka kama sekta nyeti zingine
Je tuna waalimu wenye taluma
Na leseni za juu kutoka FIFA?
Na je shuleni michezo ni lazima
Kwa maana umeitashume tena umeseta
Na mwisho kabisa
Nchi yako ina viwanja bora na academy za kutosha
Big NO definitely
Mafanikio ya chochote ni maandalizi toka chini
Acheni kuchekesha GROW UP!
Nilichoamua ni kumwamini Mungu tu
Ila kumwamini mwanadamu mwenzangu sitaki
Tena huo ni unafiki
Mtumishi wa mungu kutufundisha mema
Huku kwa simu yake kajaza pornography
Wizi, GROW UP!
Mnadhani nawahofia? Hapana
Msichokijua ni kuwa nahofia anopheles
Ndio maana kabla ya kulala nakishukisha chandarua
Na nangoja tu niwajuze
Wa kumsimamisha roma sio stamina
Ni Napoly, Inter Milan au Juve trust me
Kibaya ni kuwa tumezaliwa
Kwenye nchi ambayo wasomi wako mtaani
Ndio maana mi niliamua tu
Kuingia madrasa kuhifadhi Bible na Quran
Kizazi cha fall kizazi cha Instagram
Kizazi cha facebook, kizazi cha WhatsApp
Kizazi cha Twitter, kizazi cha Telegram
Kizazi cha Smartphone, make-up na fashion
Za kim kardashian na Migos ndio kizazi cha vigoma
Na ndio kizazi cha zero nadhani wote mnakiona
Na ndio maana kila siku tutazidi
Kuzalisha akina Amber Ruty wengi
Tena under age kuitaka ndoa
Wakati huwezi kumpikia hata mume uji
Muungwana humpongeza muungwana akifanya vya maana
Watumishi hewa walifyekwa safi
Barabara safi, treni ya mwendo kasi na fly over
Bado tu serikali ya viwanda, ajira kwa vijana
Kupanda mishahara kwa walimu na polisi
Ndio vitu tunavyoongoja
Tumeitupa Bongo fleva na kuiga sound ya Nigeria
Au mi ndo sijajuwa pengine
Bongo fleva is a type of Nigerian music, I don’t know
Mpaka sasa mtaani ni msoto
Na sijakutana na what is Biology?
Mpaka naamini huo ni uzushi
Labda study za kazi
Kidogo imenisaidia kuwa fundi Washi
Bahati mbaya mi sio mwarabu sina kitu cha kurithi
Mtaniua bure babangu ni masikini, mamangu ni masikini
Na hata kwetu kijijini nilichoachiwa
Sio mali za ng’ombe sabini
Ila nimeachiwa utajiri kichwani
Kuwa this time tomorrow ni past like a shadow
GROW UP!
Ubinafsi ndio kitu nilicho nyimwa
Nyinyi si mlizipandisha na muungo wa Utuhui Stars
Njombe Mji Lipuli, Maji Maji na Ndanda
Mimi nitazipandisha Nyasubi FC, Kahama United
Stand United, Mbanga FC, Rhino Rangers
Toto Africans, Pamba na Gwambira
Guess what?
Mi sikuzaliwa nje ya ndoa, La hasha
Ndio maana nawaheshimu sana wanawake
Ndio maana naogopa kuwachezea na kuwazalisha
Na kuwatelekeza na niishie kuwatia
Yaani kuwatia dosari na kuwatia doa
Asa kumbe hata iwe ni msoto
Iwe changamoto rijali hakatai mtoto
Mkamatwa na ngozi si ndio mla nyama
Asa mbona mnawahanya?
Mwenyekiti wa chama tawala na mgogoro
Mzito na mwenyekiti wa chama pinzani(Mschweeew)
Jamani punguzeni ushabiki kitu haukijui unakausha
Maana sisi hasa wengi wetu hatuna uelewa kuhusu siasa
Sijajuwa ni uzembe wa mzazi
Uuzembe wa walimu au ni mfumo wa elimu
Ndio unasababisha kumkuta mtoto wa darasa la tano
Hajui kusoma wala kuandika, globalization
Mtakuwa wajinga mpaka lini?
Kuunga megabytes kwa ajili ya kufuatilia
Udaku, picha chafu za video za Sanchoka
Nagundua tunapokwenda ni mbali sana kuliko tulipotoka
GROW UP!
Ni utandawazi au ni uzembe ulifanywa na wazazi
Sasa ivi ni kawaida kumkuta kijana
Mwenye umri wa miaka thelathini
Kuishi kwa wazazi
GROW UP!
Nawawashia green lights
Taifa la mbumbumbu kushadadia mambo
Na ndo maana kwenye ngoma serious
Kama hizi utakuta dislikes
Kuwasaida hawa sio kuwapa laki mbili
Bali kuwasaidia hawa ni kuwafanyia counselling ya akili
Kabla ya kupigana kutukanana huwa
Nageuka nyuma najiuliza mi ni nani? Nimetoka wapi?
Ndoto zangu zipi?
Naweka silaha chini na kuwa mpole kwa maana
Mjini sina cha shangazi Sinza wala mjomba kwa Mtogole
Ako na watu sai wanajiuliza kwa nini Nacha hahiti
Kwa nini Nacha hawi star
Na mawe yake yanapendwa sana kwa mtaa
Nawajibu mi ni mwezi kamwe siwezi kuwa star
Guess what?
Wanawake wa sasa ingawa sio wote
Ila wengi wao wana tamaa
Hawana kinyaa wanameza matapishi
Ambayo rafiki yake kayakataa
Na ndio maana wanazidi kuambukizana
Moto sababu ya motor car
Na ndio maana vijana wengi sai
Wanatumia muda mwingi kujiremba kama mabinti
Kuwa smart kutafuta majimama ni true sio masihara
Kuliko kutumia muda mwingi kutafuta kazi
Wapate ugali ili wawe wanaenda chooni mara kwa mara
GROW UP!
Asanteni naitwa NACHA
(Bear)
Ecouter
A Propos de "Grow Up"
Plus de Lyrics de NACHA
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Vous aimeriez sûrement
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl