FID Q Tajiri Yangu cover image

Tajiri Yangu Lyrics

Tajiri Yangu Lyrics by FID Q


[ Paul Clement ]

Ewe Ewe.. tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe tajiri.. wa matajiri
Ewe  tajiri..Tajiri yangu
 
[ Fid Q ]

Lord.. ni ngumu kujua wewe uko wapi ila unajua nilipo
Ninaisaka haki kuipata ni bahati na kwa waganga siko
Vyuma vikikaza tunatangatanga kuuchanga mshiko
Na mbanga zinakwaza madada wakidanga wanabamba vifo
Na waliopinda wewe huwalinda na love
Ka wale wajinga ambao hunipinga ninapouwinda wokovu
 Haunipi shida bila namna ya kuisolve
Wewe ndio mmiliki wa kila tiba na hauna iliyo mbovu

Hauna iliyombovu..
Unanipa uinchaji na power
Unaninyanyua juu
Ni zaidi ya dawa.. sikuhitaji ninapougua tu
Unaniweka sawa.. devil akitua hamchukui Q
Una uwezo wa kunigawa au kuniumbua
Sio tu kuniumba mkuu
Ni rhumba tu ndio linaweka vumba juu na nakututesa
kama mfungwa anayechungwa nakudundwa juu

Wewe ndio BOSS ninayekuamini
haututosi tukichomewa
sio wale wanaowahi kazini ili wafoke tukichelewa

[ Paul Clement]
Ewe Ewe.. tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe tajiri.. wa matajiri
Ewe  tajiri..Tajiri yangu

[ Fid Q ]
Mwanadamu amemtawala mwanadamu kwa kumuumiza
Anakwapua mpaka asivyovihitaji bila kubakiza
Hii inafanya nafsi yangu ikose subira
Ikose usingizi, uoga., huzuni na hasira
kwangu furaha ni kuwa na Mungu sio mlungura
Na pia siku zote mla raha na uchungu hula
Ninajua nilipotoka na ninajua wapi nilipo
Ispokuwa ni wewe pekee unajua lini nitafika mwisho

cheo chako ni kirefu zaidi ya dunia
Kipana zaidi ya bahari
Ulinzi mkali hakuna Askari anayefikia
Ninamlaani shetani kiundani nipate kukujua mkuu
Ili nijihami na mtihani nisiache tusua Q
Ninajua una huruma naomba nikibuma usinitose
Mwanadamu atazingua.. heshima sio utumwa kwa boss
Hawezi nunua uhai.. anajidai kwa lipi
Na kwako sio tu akeshaye hata alalaye humpa riziki..

[ Paul Clement ]
Ewe Ewe.. tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe tajiri.. wa matajiri.
Ewe  tajiri..Tajiri yangu

Siwezi kuwa masikini sababu
Anayenitunza ni tajiri.. ni Mungu
Asiyeacha nigange njaa, nikosee furaha
Nikate tamaa
Eeh wee eeh, wee tajiri yangu

[ Paul Clement]
Ewe Ewe.. tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe tajiri.. wa matajiri..
Ewe  tajiri..Tajiri yangu

 

Watch Video

About Tajiri Yangu

Album : KitaaOLOJIA (Album)
Release Year : 2020
Added By : Afrika Lyrics
Published : Aug 13 , 2020

More FID Q Lyrics

FID Q
FID Q
FID Q

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2023, We Tell Africa Group Sarl